| Swahili
ULIMWENGU
2 DK KUSOMA
Marekani yaitaka Israeli ipunguze mashambulizi dhidi ya Hezbollah ya Lebanon
Mashambulizi ya Israeli dhidi ya Gaza yameingia siku ya 259 yakiwa yameua Wapalestina 37,431, wengi wakiwa ni wanawake na watoto na kujeruhi 85,653, huku zaidi ya 10,000 wakihofiwa kuwa wamefunikwa na na vifusi vya nyumba zilizolipuliwa.
Marekani yaitaka Israeli ipunguze mashambulizi dhidi ya Hezbollah ya Lebanon
Moshi ukitoka katika baadhi ya majengo yaliyolipuliwa na Israeli katika kijiji cha Khiam, kusini mwa Lebanon jirani na mpaka na Israeli. / Picha: AFP   / Others

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewajulisha maofisa wa Israeli umuhimu wa kusitisha mashambulizi zaidi dhidi ya Lebanon na Hezbollah.

Blinken alikutana mshauri wa usalama wa Israeli Tzachi Hanegbi na Waziri wa Masuala ya Kimkakati Ron Dermer, imesema ofisi ya Mambo ya Nje katika taarifa yake.

Akisisitizia "dhamira ya dhati" ya Marekani kwa usalama wa Israel, Blinken alijadili juhudi zinazoendelea za kufikia usitishaji vita huko Gaza na kuhakikisha kuwa mateka wote wanaachiwa.

"Waziri alisisitiza haja ya juhudi za ziada za kuongeza misaada ya kibinadamu katika eneo la Gaza na ujenzi mpya wa eneo hilo," taarifa hiyo iliongeza.

Mkutano huo umekuja baada ya jeshi la Israel kusema kuwa limeidhinisha mipango ya operesheni ya mashambulizi dhidi ya kundi la Hezbollah la Lebanon ambalo limetuma ndege zisizo na rubani nchini Israel katika kipindi cha miezi minane iliyopita, huku kikishambuliana kwa mabavu na wanajeshi wa Israeli.

Pata habari zaidi kupitia whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika