| Swahili
ULIMWENGU
2 DK KUSOMA
Mpiga picha wa TRT Arabi apoteza mguu katika shambulio jipya la Gaza
Mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza yamefikia siku ya 189, na kuua wapalestina 33,545 huku 76,094 wakiwa wamejeruhiwa, wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likishindwa kuafikiana kuhusu ombi la Palestina kupata uanachama wa chombo hicho.
Mpiga picha wa TRT Arabi apoteza mguu katika shambulio jipya la Gaza
Israel ililenga kikundi cha waandishi wa habari katika eneo la Gaza, Ijumaa mchana, na kujeruhi wafanyakazi wawili wa TRT Arabi, ambapo mmoja alipoteza mguu wake (Picha: AA)  / Others
12 Aprili 2024

Waandishi wawili wa habari wa TRT Arabi wamejeruhiwa katika shambulizi jipya la Israel siku ya Ijumaa mchana katika kambi ya Nuseirat katikati mwa Gaza. Mpiga picha Sami Shehadeh alijeruhiwa vibaya huku madaktari wakilazimika kuukata mguu wake wa kulia.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Jeshi la Israel lililenga kundi la waandishi wa habari, ikiwa ni pamoja na timu ya Kiarabu ya TRT, waliokuwa wakiripoti kutoka kambi ya wakimbizi ya Nuseirat. Baadhi ya waandishi wa habari walijeruhiwa baada ya kusmabuliwa na kifaru cha Israel.

Mwakilishi wa TRT Arabi Sami Berhum na waandishi wengine pia walijeruhiwa kwenye tukio hilo.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Gaza, waandishi wa habari wasiopungua 140 wamepoteza maisha katika mashambulizi ya Israel huko Gaza.

Siku ya jana, Jeshi la Israel lilitangaza kuanzisha "operesheni ya kushtukiza" katikati mwa Gaza, na kusababisha mauaji ya Wapalestina wengi.

Mkurugenzi Mkuu wa TRT, Zahid Sobaci alilaani shambulio hilo, na kulielezea kama "ukatili" usio na "kikomo cha maadili, kisheria au kibinadamu."

CHANZO:Reuters