| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Idadi ya walioambukizwa Ebola nchini DRC yazidi 12,000
Kwa sasa hakuna matibabu au chanjo iliyoidhinishwa kutibu virusi hivyo.
Idadi ya walioambukizwa Ebola nchini DRC yazidi 12,000
Idadi ya walioambukizwa Ebola DRC inazidi kuongezeka / Reuters (Wire)
 

Idadi ya maambukizi ya Ebola yaliyothibitishwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imevuka 12,000, kulingana na takwimu za serikali zilizotolewa Novemba 26.

Jumla ya maambukizi yaliyothibitishwa ni 12,021 na waliofariki ni 5,904.

Mlipuko huo, unaosababishwa na virusi aina ya ‘Bundibugyo,’ ulitangazwa katikati ya mwezi Mei katika mkoa wa Ituri, kaskazini-mashariki mwa DRC, na tangu wakati huo umeenea katika mikoa minane kati ya mikoa 26 ya nchi hiyo.

Kwa sasa, hakuna matibabu au chanjo iliyoidhinishwa kutibu virusi hivyo.

Kuchelewa kugunduliwa kwa ugonjwa huo, migogoro inayoendelea, na kulemewa kwa huduma za afya, vinatajwa kuchangia kuenea kwa kasi kwa maambukizi tofauti na milipuko iliyopita.

Huu ni mlipuko wa pili kwa ukubwa na wa pili kusababisha vifo vingi katika historia, ukifuatia ule uliotokea Afrika Magharibi kati ya mwaka 2014 na 2016, ambapo zaidi ya watu 28,600 waliambukizwa na zaidi ya 11,000 kufariki.

CHANZO:Reuters (Wire)