ULIMWENGU
1 dk kusoma
Israel yafanya mashambulizi ya anga dhidi ya Gaza na kukiuka makubaliano ya kusitisha vita
Ndege za Israel zimeshambulia mji wa Gaza, walioshuhudia wanasema, mashambulizi hayo yamejiri muda mfupi tu baada ya Netanyahu kuamuru jeshi la Israel kufanya mashambulizi makali.
Israel yafanya mashambulizi ya anga dhidi ya Gaza na kukiuka makubaliano ya kusitisha vita
Israel yashambulia kambi ya al-Shati magharibi mwa jiji la Gaza , na kukiuka usitishaji mapigano, mwandishi wa Anadolu anaripoti. / / AFP
tokea masaa 11

Israel imefanya takriban mashambulizi matatu ya anga katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, mara tu baada ya agizo hilo la Netanyahu kutolewa. Kwa mujibu wa shirika la uokoaji la kiraia la Palestina katika Ukanda wa Gaza

“Jeshi la uvamizi sasa linashambulia Gaza kwa takriban mashambulizi matatu ya anga licha ya makubaliano ya usitishaji mapigano,” alisema msemaji wa shirika hilo, Mahmud Bassal, akizungumza na shirika la habari la AFP.

Walioshuhudia mashambulizi hayo wamesema milio ya mizinga na milipuko imesikika na kuonekana katika Jiji la Gaza na maeneo mengine ya ukanda huo.

CHANZO:TRT World