| swahili
AFRIKA
3 DK KUSOMA
Sudan: 'Ikiwa majenerali wa mapigano watamsikiliza Salva Kiir, hali ya kawaida itarejea ndani ya saa moja'
Mwakilishi wa Sudan Kusini katika Umoja wa Afrika anaiambia TRT Afrika kwamba Rais Kiir anapaswa kupewa nafasi ya kuketi na Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fatah al-Burhan na kamanda wa kikosi cha Rapid Support Forces Mohamed Hamdan Dagalo
Sudan: 'Ikiwa majenerali wa mapigano watamsikiliza Salva Kiir, hali ya kawaida itarejea ndani ya saa moja'
Vurugu za Sudan zinaendelea licha ya kutangazwa kwa makubaliano / Picha: AA
28 Aprili 2023

Mwakilishi wa Kudumu wa Sudan Kusini katika Umoja wa Afrika ametoa wito kwa vikosi vya mapigano nchini Sudan kuja kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza ghasia zinazoendelea nchini humo.

Katika mahojiano maalum na TRT Afrika Swahili, Balozi James Pitta Morgan alisema rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir ana uwezo wa kupatanisha na kumaliza ghasia hizo akiwataka majenerali wawili wanaoongoza vita vya kuwania madaraka kumsikiliza.

''Ikiwa majenerali hao wawili watatupa nafasi ya kumsikiliza rais wangu hali ya Sudan itakuwa sawa moja kwa moja,'' balozi Peter Morgan alisema kwenye mahojiano Ijumaa.

Aliwataja al Burhan na Hamdan Dagalo maarufu kama Hemedti kama ''ndugu'' ambao wanapaswa kuketi kwa ajili ya mazungumzo.

Mjumbe wa Sudan Kusini alisema ikiwa majenerali hao ''wanaweza kumpa rais wangu saa moja tu, kukaa nao, wote wawili, nadhani wote watakubaliana.''

Aliongeza kuwa Sudan na Sudan Kusini wana muhimu kimkakati kwa kila mmoja kwa sababu ya historia yao na dhamana. Sudan Kusini ilipata uhuru kutoka kwa Sudan mwaka 2011.

Juhudi kadhaa za kimataifa katika siku za hivi karibuni za kupatanisha majenerali hao wawili haijazaa matunda na matokeo yoyote ya kimaendeleo yanayoheshimiwa na wahusika.

Wiki iliyopita, Muungano wa maendeleo wa Afrika Mashariki na pembe ya Afrika, IGAD, walitangaza kuwa rais wa Kenya, Djibouti na Sudan Kusini wameteuliwa kwa ajili ya maongezi na Sudan.

Jeshi la Sudan lilikuwa limetangaza Jumatano kuwa limetoa ''kibali cha awali'' cha mazungumzo katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba na RSF na wajumbe kutoka pande hizo mbili wakitarajiwa kukutana. Hadi sasa, kidogo kimesikika kuhusu maendeleo ya mipango hayo.

Mwakilishi wa Sudan Kusini Umoja wa Afrika alisema kwa kawaida ''mapigano yanapoendelea, watu hawataki kusikilizana'' akiongeza kuwa ni wakati wa majeshi yanayozozana nchini Sudan kuja kwenye meza ya mazungumzo.

Mapigano nchini Sudan yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 400. Imesababisha raia wa Sudan kuhamia nchi jirani na kuendelea kuwahamisha raia wa kigeni.

A ceasefire agreed by the two parties was extended Thursday might just before it expired. But sporadic violence was reported Friday morning.

Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyokubaliwa na pande zote mbili yaliongezwa Alhamisi, kabla ya muda wake kuisha. Lakini vurugu za hapa na pale ziliripotiwa Ijumaa asubuhi.

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
UN yaagiza uchunguzi wa dharura ufanyike kuhusu ukiukaji wa sheria katika Al Fasher ya Sudan
Rais wa Tanzania atangaza uchunguzi kuhusu mauaji ya waandamanaji katika uchaguzi
Wakimbizi 57,000 wamewasili kaskazini mwa Sudan baada ya mashambulizi ya RSF huko Darfur, Kordofan
Afrika Kusini yaruhusu kuingia kwa wakimbizi zaidi ya 150 kutoka Gaza, Palestina
Afrika yakumbwa na mlipuko wa kipindupindu mbaya zaidi katika miaka 25
Mataifa ya G7 walaani mashambulizi ya RSF dhidi ya raia Sudan, watoa wito wa kusitishwa mapigano
Wakenya zaidi ya 200 wajiunga na jeshi la Urusi
AU yakanusha tuhuma za Trump kuhusu mauaji ya halaiki Nigeria
Mwigulu Nchemba ateuliwa Waziri Mkuu Tanzania
Jaji Mkenya achaguliwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amfuta kazi makamu wake
Duma wa Botswana aipa India zawadi ya duma 8
Kesi ya Roger Lumbala wa DRC yaanza kusikilizwa
Kesi za ubakaji, watoto kupotea zaripotiwa Darfur, Sudan – Umoja wa Mataifa
Ugonjwa wa Kichaa cha mbwa barani Afrika: Janga linaloendelea kuathiri maisha japo linaepukika
Libya yatakiwa kufunga vituo vya kuwazuilia wahamiaji katika mkutano wa Umoja wa Mataifa
Rais Museveni aonya kuzuka kwa vita endapo nchi za Afrika zitashindwa kufikia Bahari ya Hindi
UN: Milioni 11 wanawake na wasichana wanabeba uzito mkubwa wakati njaa ya Sudan inaendelea kupamba moto
Ethiopia yachagguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa, COP32
Ghana yafichua sababu ya ajali ya helikopta iliyoua watu wanane, wakiwemo mawaziri, mwezi Agosti