AFRIKA
2 DK KUSOMA
Rais wa Sudan Kusini akubali kuongea na upinzani kabla ya uchaguzi
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amekubali kufanya mazungumzo na upinzani kabla ya uchaguzi wa Desemba 2024.
Rais wa Sudan Kusini akubali kuongea na upinzani kabla ya uchaguzi
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ameweka Disemba 2024 kuwa tarehe ya uchaguzi mkuu wa kwanza nchini humo. / Picha: AA / Others
28 Machi 2024

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemuomba Rais wa Kenya William Ruto kutuma mpatanishi ambaye atashiriki katika kile anachokiita Mchakato wa Usuluhisho wa Amani huko Sudan Kusini.

Kupitia taarifa kutoka kwa Msemaji wa Ikulu ya Kenya Hussein Mohamed, Kiir aliomba mazungumzo hayo yafanyike ili pande zote za serikali tawala na upinzani ziweze kutatua masuala yenye utata kabla ya uchaguzi wa Desemba.

Hii imetokea baada ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar kuomba duru mpya ya mazungumzo kabla ya uchaguzi kufanyika, akisema maendeleo madogo yamefanyika kuhakikisha uchaguzi wa Desemba unakuwa wazi.

"Mazungumzo yanalenga kufikia makubaliano na amani kuelekea uendeshaji wa uchaguzi (wa Desemba)," Mohamed alisema katika taarifa siku ya Alhamisi.

Nyongeza ya Muda

Machar alipendekeza muda wa serikali ya mpito uongezwe ili kuruhusu maandalizi ya kutosha kwa ajili ya uchaguzi, lakini upande wa Kiir umekataa wito wa upanuzi.

Kenya imewateua Kamanda wa Jeshi la Zamani Lazarus Sumbeiywo na Balozi Mohammed Ali Guyo kuongoza mazungumzo hayo.

Pata habari zaidi kupitia whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika