AFRIKA
2 DK KUSOMA
Kampuni ya Uturuki ya BOTAS yaingia mkataba wa gesi asilia na ExxonMobil ya Marekani
Kampuni ya serikali ya BOTAS imeingia makubaliano na ExxonMobil kwa lengo la kupanua rasilimali za nishati na kuongeza usalama wa usambazaji wa kikanda.
Kampuni ya Uturuki ya BOTAS yaingia mkataba wa gesi asilia na ExxonMobil ya Marekani
Uturuki inalenga kuwa kitovu cha gesi asilia. / Picha: AA   / Others
9 Mei 2024

Shirika la Bomba la Petroli la Uturuki (BOTAS) na kampuni ya nishati ya Marekani, ExxonMobil, zimetia saini mkataba wa ushirikiano kuhusu biashara ya gesi ya kimiminika (LNG), Waziri wa Nishati na Maliasili wa Uturuki ametangaza.

"Kwa makubaliano haya, ambayo yamepangwa kuwa ya muda mrefu, tutachukua hatua nyengine katika kubadilisha rasilimali zetu," Alparslan Bayraktar aliandika kwenye mtandao wake wa X kufuatia kutiwa saini Jumatano, wakati wa ziara ya Washington, DC.

"Sisi ni miongoni mwa nchi chache duniani zenye uwezo wetu wa kutengeneza gesi," alisema, na kuongeza kuwa Uturuki "itaendelea kuchangia usalama wa usambazaji wa nishati ya nchi yetu na katika kanda yetu kwa ujumla."

Kulingana na Waziri huyo, mwezi uliopita Uturuki ilikuwa na mazungumzo na ExxonMobil kupata tani milioni 2.5 za gesi hiyo yenye thamani ya karibu dola bilioni 1.1, katika mkataba utakaodumu kwa miaka kumi.

Uturuki ina mabomba saba ya kimataifa ya gesi asilia, vitalu vitano vya gesi hiyo vikihusisha vitatu vyenye kuelea majini na viwili vya kuhifadhi gesi asilia chini ya ardhi.

Nchi hiyo inalenga kuwa kitovu cha gesi asilia katika kanda, hatua itakayoiwezesha kuiuza nje ya nchi.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika