| Swahili
ULIMWENGU
2 DK KUSOMA
Idadi ya vifo vya Wapalestina yafikia 36,439, Israeli ikiua zaidi ya 60 huko Gaza
Kulingana na Wizara ya Afya, Wapalestina 220 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Israeli ndani ya saa 24.
Idadi ya vifo vya Wapalestina yafikia 36,439, Israeli ikiua zaidi ya 60 huko Gaza
Taarifa kutoka Wizara ya Afya imesema kuwa Wapalestina wengine 82,627 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo./Picha: AA / Others

Wapalestina wapatao 36,439 wameuwawa katika mashambulizi yanayoendelea katika ukanda wa Gaza, tangu Oktoba mwaka jana, Wizara ya Afya katika eneo hilo imesema.

Taarifa ya Wizara ya Afya iliongeza kuwa watu wengine 82, 627 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo.

“Mashambulizi ya Israeli yameua watu 60 na kujeruhi wengine 220 ndani ya saa 24,” taarifa hiyo imesema.

“Watu wengi bado wamefunikwa na vifusi huku waokoaji wakipata shida kuwafikia,” imebainisha.

Miezi nane tangu kutokea kwa mashambulizi hayo, mji wa Gaza umegeuka kuwa vifusi vya nyumba, huku kukiwa na vizuizi vikubwa vya upatikanaji wa chakula, maji safi na dawa.

Israeli inashutumiwa na kwa mauaji ya "kimbari" katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ambayo katika uamuzi wake wa hivi karibuni, iliitaka Tel Aviv kusitisha mara moja operesheni zake katika eneo la Rafah lililo kusini mwa Gaza.

Pata habari zaidi kupitia whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika, AA