| Swahili
ULIMWENGU
1 DK KUSOMA
Wapalestina wauwawa katika shambulizi la shule mjini Gaza
Mauaji ya kimbari ya Israeli dhidi ya Gaza yameingia siku ya 302, yakiwa yameua Wapalestina 39,550, wengi wakiwa ni wanawake na watoto, na kujeruhi zaidi ya 91,280.
Wapalestina wauwawa katika shambulizi la shule mjini Gaza
Jeshi la Israeli limelipua chuo katika mji wa Gaza./ Picha: AA   / Others

Wapalestina 10 wameuwawa katika shambulio la shule iliyokuwa imehifadhi watu wasio na makazi katika eneo la Sheikh Radwan lililoko Gaza, kitengo cha habari kimesema.

Kulingana na kikosi cha Ulinzi wa raia cha Gaza, shambulio hilo lililotekelezwa na Israeli, liliua Wapalestina 10 katika eneo la shule.

"Kuna mashahidi 10 na majeruhi wengine wengi kufuatia mashambulizi ya Israeli katika shule ya Hamama," msemaji wa kikosi hicho Mahmud Bassal aliiambia AFP.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika