3 Oktoba 2025
Namibia na Zimbabwe wamejihakikishia nafasi zao kwenye Kombe la Dunia la Kriketi T20 mwaka 2026 baada kutinga fainali za kanda ya Afrika mjini Harare siku ya Alhamisi.
Timu zote mbili zimefuzu kwa mashindano ambayo yatakuwa na wenyeji wenza India na Sri Lanka kati ya mwezi Februari na Machi mwakani.
Zilizopendekezwa
Namibia iliifunga Tanzania kwa mikimbio 63 katika nusu fainali iliyokuwa na msisimko mkubwa. Zimbabwe nayo ikaigaragaza Kenya katika uwanja wa nyumbani Harare na kuwa timu ya 17 kufuzu kwa Kombe la Dunia T20 mwaka 2026.
Namibia na Zimbabwe watapambana kwenye fainali ya Kanda ya Afrika Oktoba 4, lakini timu zote mbili zimefuzu kwa mashindano ya Kombe la Dunia.
CHANZO:TRT Afrika Swahili