Bado kuna nafasi tatu za kuwania kwa ajili ya Kombe la Dunia 2026.
Hatua hii ya mashindano ya muondoano yatahusisha timu moja kutoka kila shirikisho litakuwa na timu moja (isipokuwa UEFA), na timu moja zaidi kutoka kwa shirikisho wenyeji la CONCACAF, kwa kuwa Kombe la Dunia litakuwa na wenyeji wenza Canada, Mexico na Marekani.
Timu nne kutoka bara la Afrika zimeingia hatua hiyo nazo ni Nigeria, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Gabon.
Mechi hizo za Afrika zitafanyika nchini Morocco kuanzia Novemba 13 hadi 16. Mashindano haya yatakuwa na mfumo wa muondoano, na baadaye kucheza nusu fainali na kumalizika na fainali kuamua nani mshindi
Mshindi wa mashindano haya madogo ataelekea kucheza michuano kati ya mashirika tofauti, ili kutafuta nafasi zilizobaki na Kombe la Dunia.
Kwa hiyo shirikisho la CONCACAF litakuwa na timu mbili katika hatua hii, huku mashirikisho ya AFC, CAF, CONMEBOL na OFC wakitarajiwa kupata nafasi moja moja.
Kutakuwa na mashindano mengine kati ya timu hizi. Kulingana na nafasi zao za ubora timu hizo za taifa zitacheza fainali mbili. Kutakuwa na mechi za muondoano na kisha nusu fainali.
Timu zitakazoibuka washindi kwenye fainali hizi ndizo zitakazojaza nafasi mbili za Kombe la Dunia.