Baadhi ya timu zinazocheza katika Ligi Kuu ya England zilikuwa zinafurahia matokeo yao ya Ligi Kuu ya Mabingwa Ulaya huku wengine wakitafakari mbinu watakayorejea nayo kwenye mechi zao zinazofuata.
Arsenal sasa imepata ushindi kwenye mechi zake mbili baada ya kuwafunga Olympiacos 2-0.
Meneja wa Arsenal Mikel Arteta alipongeza vijana wake kwa ujasiri na kujituma katika kujihakikishia ushindi huo.
Manchester City hawakuwa na bahati baada ya wapinzani wao Monaco kupata penati ya dakika za mwisho na kulazimisha sare ya 2-2. Ni mara ya tatu msimu huu kwa wao kupoteza alama dakika za mwisho mwisho.
Newcastle ilipata ushindi wake wa kwanza katika Ligi ya mabingwa barani Ulaya, ikiwa ni ushindi wa kwanza ugenini tangu 2003. Waliifunga Union Gilloise ya Ubelgiji 4-0
PSG iliwafunga Barcelona 2-1 huku Dortmund ikiwacharaza Athletic Bilbao magoli 4-1.