Mchezo wa Kimataifa wa mbio za Ngamia za Maralal ni moja kati ya michezo adimu sana nchini Kenya.
Ngamia wanashindana kuanzia mwanzo wa maji huo, wakiwa wakakamavu.
Mashabiki wakiwa makini kwenye njia zenye vumbi, wengi wakiwa wamevaa shanga zao za asili zenye rangi nyekundu, bluu na njano huku jua likichomoza.
Kila mwezi Septemba, mji mkuu wa Kaunti ya Samburu kaskazini mwa Kenya kuna tamasha la siku tatu la mbio za ngamia ambalo linawaleta pamoja waendeshaji waliobobea, chipukizi, na watalii kushuhudia hafla ambayo ni ya kipekee na yenye burudani.
Tamasha la mwaka huu lilifanyika Septemba 25 hadi 28, na limeadhimisha mashindano ya 32 ya kila mwaka.
Ushindani mkubwa
Ushindani mkubwa uko katika madaraja mawili.
Wale waliobobea wanashindana katika mbio za kilomita 20, huku mshindi akiondoka na shilingi 80,000 za Kenya ($617), wa pili akipata shilingi 60,000 ($463), na watatu akitia kibindoni shilingi 40,000 ($310).
Washindani chipukizi wanashindana katika mbio za kilomita 10 kwa zawadi ya fedha za shilingi 70,000 ($540), shilingi 50,000($388), na shilingi 40,000 ($310) kwa mshindi wa kwanza, wa pili na watatu, mtawalia.
Arne Selengubaya ameshiriki katika mashindano ya Maralal kwa zaidi ya miongo miwili, na kila wakati inakuwa tofauti.
Mshiriki mwingine ni Emmanuel Labartengat ambaye anaamini kuwa mashindano hayo ni zaidi ya zawadi ya fedha, mandhari yake inavutia. "Tunapenda mbio za ngamia, na fedha ni nyongeza. Uwepo wa watalii kunafanya mashindano hayo kuwa na mvuto zaidi," ameiambia TRT Afrika.
Yanaunganisha watu
Viongozi wa jamii na wanaopigia chapuo mashindano hayo ambayo ni zaidi ya kivutio cha utalii tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990.
Kile ambacho kimekuwa mashindano ya msimu kwa ajili ya jamii za maeneo hayo tu sasa kimekuwa sehemu muhimu inayowakilisha kaskazini mwa Kenya.













