| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Mahakama ya Ufaransa yaiamuru PSG kumlipa Mbappe zaidi ya dola milioni 70
Mahakama ya Ufaransa imeiamuru klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) kumlipa mshambuliaji Kylian Mbappé zaidi ya dola milioni 70 kutokana na mishahara na posho ambazo hakulipwa.
Mahakama ya Ufaransa yaiamuru PSG kumlipa Mbappe zaidi ya dola milioni 70
Akiwa na umri wa miaka 26 pekee, Mbappe tayari ni mshindi wa Kombe la Dunia na mmoja wa washambuliaji wakuu wa soka. / / AFP
tokea masaa 13

Mahakama ya ajira ya Paris ilitoa uamuzi huo siku ya Jumanne, ikisema PSG ilishindwa kumlipa Mbappé mishahara ya miezi mitatu pamoja na posho ya maadili na bonasi ya kusaini mkataba. Uamuzi huo umemaliza sehemu ya mgogoro uliodumu kwa miezi kadhaa kati ya mchezaji huyo na klabu hiyo, mgogoro uliotikisa soka la Ufaransa.

Mbappé aliifungulia PSG kesi akidai kuwa mishahara yake ya miezi ya Aprili, Mei na Juni 2024 ilizuiwa kimakusudi, muda mfupi kabla ya kuondoka timu hiyo na kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bila malipo.

“Tumefurahishwa na uamuzi wa mahakama. Hizi ndizo hatua zinazotarajiwa pale mishahara inapokosa kulipwa,” alisema wakili wa Mbappé, Frederique Cassereau.

Mahakama ilibaini kuwa PSG ilikiuka mkataba wake wa ajira kwa kutomlipa Mbappé mishahara ya miezi mitatu, posho ya maadili na bonasi ya kusaini mkataba. Malipo hayo yalikuwa tayari yamethibitishwa kuwa yanatakiwa kulipwa kupitia maamuzi mawili ya Ligi ya Soka ya Kulipwa ya Ufaransa (LFP) yaliyotolewa Septemba na Oktoba 2024.

Majaji pia walieleza kuwa PSG haikuwasilisha ushahidi wowote wa maandishi unaoonyesha kuwa Mbappé alikubali kuachana na haki yake ya kupokea malipo hayo.