| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Rais Ruto amkaribisha Rais Mnangagwa wa Zimbabwe nchini Kenya
Kenya na Zimbabwe kufanya mkutano wa kwanza wa Tume ya Pamoja ya Kitaifa (BNC).
Rais Ruto amkaribisha Rais Mnangagwa wa Zimbabwe nchini Kenya
Kenya na Zimbabwe pia zinalenga kuongeza biashara ya pande mbili kufikia Dola milioni. /Ikulu / X
 

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, yuko nchini Kenya kwa ziara rasmi ya siku mbili, ambapo amekutana na mwenyeji wake, Rais William Ruto, katika Ikulu kwa mazungumzo yanayolenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Katika ziara hiyo, viongozi hao watajadili masuala mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji.

Aidha, mkutano wa kwanza wa Tume ya Pamoja ya Kitaifa (BNC) unatarajiwa kufanyika kwa lengo la kuweka mikakati ya kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu.

Kenya na Zimbabwe pia zinalenga kuongeza biashara ya pande mbili kufikia Dola milioni 70 za Marekani kwa mwaka, hatua inayotarajiwa kufungua fursa zaidi za kiuchumi, uwekezaji na ajira kwa wananchi wa mataifa hayo.