Jiji la Antalya limepokea watalii milioni 14 toka kuanza kwa mwaka 2026, licha ya changamoto za mgogoro wa Mashariki ya Kati na vita kati ya Urusi na Ukraine.
Kulingana na rais wa Chama cha Mawakala wa Utalii na Wamiliki wa Mahoteli katika ukanda wa Mediterenea (AKTOB) Kaan Kasif Kavaloglu, msimu huu wa utalii umekuwa na mchango mkubwa, licha ya masuala mbalimbali yanayoendelea ulimwenguni.
Kavaloglu alibainisha kuwa, sekta hiyo ya utalii hiyo imefanikiwa kustahimili changamoto ya miaka mitano, ya vita vya Urusi na Ukraine, huku asilimia kubwa ya wageni wakitokea nchini za Ukraine, Hungaria na Uzbekistan.
“Kwa sasa, gharama ni za nafuu zaidi kuliko ilivyokuwa mwezi Julai na Agosti,” alisema.
Kulingana na Kavaloglu, mji wa Antalya upo tayari kwa maandalizi ya Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi, utakaofanyika mwezi Novemba.





















