Djibouti inaendelea, japo kwa taratibu, ahueni ya kweli kidiplomasia katika eneo la Pembe ya Afrika.
Katika ngazi ya Umoja wa Afrika, Djibouti inaendelea kuunga mkono jitihada za usuluhishi.
Nchi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kutatua migogoro iliyoikumba maeneo tofauti kama vile Sudan, Somalia, Ethiopia na mwambao wa Bahari ya Shamu.
Mara kwa mara, Djibouti imekuwa mjumbe katika Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, ikiwemo mwezi Machi 2025.
Diplomasia ya kanda na usuluhishi
Kwa sasa, Djibouti ndipo yalipo makao makuu ya IGAD.
Mara kadhaa, nchi hiyo imehusika katika usuluhishi wa migogoro ya kikanda.
Kwa mfano, iliwahi kuwa mwenyeji na mdhamini wa kikao cha maridhiano cha Arta Somali kilichofanyika mwaka 2000 na kuanzisha serikali ya sasa nchini Somalia baada ya kuanguka kwa utawala wa kijeshi wa mwaka 1991.
Mwaka 2008, ilisuluhisha mgogoro kati ya serikali ya shirikisho ya Somalia na sehemu ya upinzani.
Mbali na hapo, mara kadhaa, Djibouti imesuluhisha mgogoro kati ya serikali ya shirikisho na viongozi wa Somaliland.
Jitihada hizi zililenga kurejesha mazungumzo yenye maslahi kati yake na Marekani na Umoja wa Ulaya.
Hali kadhalika, Djibouti inachangia vikosi vya kulinda usalama ndani ya Somalia na imekuwa ikishiriki kupambana na kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab.
Djibouti ilijitolea kwenye kushiriki kwenye usuluhishi wa mgogoro wa Sudan.
Mwaka 2023, rais wake alishika nafasi ya uenyekiti wa IGAD, na kufanikisha mazungumzo kati ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, rais wa baraza la mpito la Sudan na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo (“Hemedti”) kutoka kikundi cha RSF.
Licha ya kuwa, mgogoro huo bado unaendelea, Djibouti inaendelea kuchechemua azimio la amani.
Kati ya mwaka 2023 na 2024, mashambulizi ya kikundi cha Wahuthi kutoka Yemen yalisababisha meli kuacha kutumia njia ya Bab el-Mandeb na Bahari ya Sham, hali iliyohatarisha uchumi wa Djibouti.
Ikitumia nafasi yake ndani ya IGAD, Djibouti imeendelea kuwa na ushawishi na yanayotokea Yemen, ikisukumwa na idadi ya wakimbizi wa Kiyemen.
Ushirikiano wa kidiplomasia kwa suluhu za kikanda
Umuhimu wa Djibouti kidiplomasia, ulikuwa dhahiri wakati ilipokuwa mwenyeji wa wa Tatu kati ya Uturuki na Afrika uliofanyika 2024.
Mwendelezo huu wa Djibouti unatoa tumaini jipya katika eneo linalokumbwa na migogoro ya mara kwa mara.
Msimamo wake kuhusu Gaza
Djibouti imekuwa na nafasi muhimu kwenye suala la Palestina.
Ilipongeza makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano, hasa jitihada zilizofanywa na Marekani, Qatar, Misri na Uturuki.
Rais Ismail Omar Guelleh alihimiza utekelezaji kamili ili kuhakikisha amani ya kudumu, misaada ya kibinadamu, na njia ya kuaminika kuelekea suluhisho la serikali mbili.
Msimamo thabiti wa Djibouti unaimarisha msimamo mpana wa Kiafrika: amani lazima itangulize upatikanaji wa misaada ya kibinadamu, kubadilishana wafungwa, na matokeo yanayowezekana ya serikali mbili huku ikilinda haki za Palestina na lengo la taifa huru la Palestina.
Mfano wa Djibouti ni wa kuigwa.
Nchi ndogo inaweza kuwa na ushawishi wa hali ya juu wakati diplomasia yake ni thabiti, ya kuaminika, na yenye msingi katika utulivu wa nyumbani.
Pembe ya Afrika bado ni tete: Vita vya Sudan vinahatarisha kuenea kwa kikanda; Mvutano wa Ethiopia-Eritrea unaendelea; Ukosefu wa usalama wa Bahari Nyekundu unatishia biashara ya kimataifa; na shinikizo la hali ya hewa huzidisha majanga ya kibinadamu.
Djibouti haiwezi kutatua changamoto hizi peke yake, lakini sauti yake kama kiunganishi na mpatanishi ni ya lazima.
Kwa kuunga mkono upatanishi unaoongozwa na Umoja wa Afrika, kuunga mkono mfumo wa usitishaji vita wa Gaza, na kutetea upatikanaji wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan, Djibouti imejiweka kama mpatanishi na kielelezo cha utulivu, huku uhusiano wake sawia na mataifa yenye nguvu duniani ukikuza ushawishi wake nje ya mipaka yake.
Hafsa Abdiwahab Sheikh ni mwandishi wa habari wa kujitegemea na mtafiti anayejihusisha na siasa za ukanda wa Afrika Mashariki.











