Rais wa Israel Isaac Herzog, amesema kuwa ombi la Waziri Mkuu wan chi hiyo Benjamin Netanyahu, kupata msamaha kwenye kesi yake ya ufisadi litazua mjadala.
Akizungumza siku ya jumatatu, Herzog alisema ombi hilo litashughulikiwa kwa uangalifu mkubwa.
“Nitazingatia maslahi ya Israel na jamii ya Waisrael,”alisema Herzog kupitia taarifa ya ofisi yake.
Kulingana na Herzog, uamuzi huo utaibua sintofahamu na hoja tofauti nchini humo.
“Ila kitu kimoja kilicho dhahiri kwangu, huwa sishawishiki na uovu wowote,” alisema Herzog.
Siku ya Jumapili, Netanyahu alimuomba msamaha rais wa nchi hiyo kwenye kesi yake ya ufisadi, huku upinzani kumtaka Herzog kutupilia mbali ombi hilo, mpaka Netanyahu akiri makosa yake.
Kwa upande wake, Rais Donald alimuombea Netanyahu msamaha kupitia Rais Herzog.
Kulingana na taarifa zilizovuja kutoka kwenye ofisi ya Netanyahu, mapitio ya msamaha huo yanaweza kuchukua wiki kadhaa za kupitiwa.
Toka kuanza kwa kesi yake, Netanyahu ameshindwa kukiri kosa lake, huku sheria za Israel zikimpa mamlaka rais kutoa msamaha iwapo mkosaji atakiri kosa lake.













