| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Mkuu wa Kupambana na Rushwa ateuliwa Waziri Mkuu Madagascar
Rais wa Madagascar, Michael Randrianirina, amemteua Mamitiana Rajaonarison kuwa waziri mkuu, siku chache baada ya kumuondoa waziri mkuu wa awali pamoja na baraza lote la mawaziri.
Mkuu wa Kupambana na Rushwa ateuliwa Waziri Mkuu Madagascar
Michael Randrianirina aliingia madarakani kama rais wa Madagascar baada ya serikali ya Andry Rajoelina kuondolewa madarakani. / Reuters
tokea masaa 5

Rais wa Madagascar Michael Randrianirina amesema siku ya Jumapili kuwa amemteua mkuu wa idara ya kupambana na rushwa Mamitiana Rajaonarison kuwa Waziri Mkuu, siku chache baada ya kumfuta waziri wake mkuu na baraza lote la mawaziri.

Randrianirina, ambae ameingia madarakani Oktoba na kuahidi mabadiliko kadhaa, amesema waziri mkuu mpya ataongoza serikali "katika njia sahihi" na kurudisha matumaini.

Hakuna kauli iliyotolewa mara moja na Rajaonarison.

"Uadilifu uliokuwa nao nautegemea kutoka kwako kama waziri mkuu. Onesha kwamba nchi inahitaji watu wenye uadilifu – watu ambao hawayumbishwi na hawawezi kununuliwa," amesema Rais katika hotuba yake kupitia televisheni.

Hakutoa sababu maalumu ya kumfuta aliyekuwa Waziri Mkuu Herintsalama Rajaonarivelo pamoja na baraza zima la mawaziri Jumatatu.

Kusuka ajenda upya

Randrianirina ameongoza kile alichokiita “kuweka msingi upya” tangu kuingia madarakani, kufuatia mabadiliko ya kisiasa ambayo yaliitoa madarakani serikali iliyopita.

Ametengeza upya ajenda kwa lengo la kurudisha mamlaka, kupambana na rushwa na kujenga imani ya wananchi.