Eritrea inatarajiwa kurudi tena kwenye michuano ya kimataifa baada ya kutokuwepo kwa zaidi ya miaka sita ilipoanza kuingia kwenye mechi za kuwania kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2027, zitakazoanza mwezi Machi.
Taifa hilo lililoko kwenye Bahari ya Shamu linatarajiwa kucheza mikondo miwili ya nyumbani na ugenini dhidi ya Eswatini mwezi Machi, ikiwa ni hatua ya awali. Mara ya mwisho kucheza mechi ya kimataifa ilikuwa dhidi ya Sudan Januari 2020.
Eritrea haijawahi kushiriki katika mashindano ya kimataifa tangu kukataa fursa katika mechi za kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia na CHAN kutokana na wachezaji kuomba hifadhi ya kisiasa mara kwa mara wanapokuwa nje ya nchi.
Eritrea ilipata uhuru wake kutoka Ethiopia 1993.
Wachezaji na maafisa wengine wa timu wameomba hifadhi baada ya mashindano nchini Angola 2007, Kenya 2009, Tanzania 2011, Uganda 2012, Botswana 2015, kufuatia mechi za kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia, na Uganda kwa mara nyingine 2019.
Kubadilisha msimamo
Inasemekena kuwa takriban wachezaji soka 80 wameomba hifadhi wakiwa katika majukumu ya timu ya taifa nje ya nchi, wote hawajaendeleza kipaji chao cha kandanda.
Eritrea haijaruhusu timu kusafiri nje ya nchi tangu wachezaji wa vijana wasiozidi umri wa 20 20 kuomba hifadhi Uganda 2019.
Hawajaorodheshwa na FIFA
Eritrea haijaorodheshwa na Shirika la Soka Duniani FIFA kwa sababu haijacheza mechi za FIFA katika kipindi cha miezi 48.
Droo ya awali ya kuwania kufuzu kwa AFCON 2027:
Djibouti v Sudan Kusini Chad v Burundi Somalia v Mauritius Ushelisheli v Lesotho Eritrea v Eswatini Sao Tome e Principe v Ethiopia. Timu iliyo ya kwanza inacheza mkondo wa kwanza nyumbani. Mechi hizo zitachezwa kati ya 25-31 Machi.














