Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametuma ujumbe wa video Jumamosi Machi 21 katika mpango wa maadhimisho ya Nowruz, akionesha matumaini kwamba tukio hilo litachangia kumaliza migogoro katika kanda.
Katika ujumbe wa tukio hilo lililofanyika katika ukumbe wa michezo wa Kamil Ocak Sports Hall katika mkoa wa kusini mashariki mwa Uturuki wa Gaziantep, Erdogan aliwapongeza wale wanaosherehekea Nowruz katika “kitovu cha utamaduni na jiografia.”
Aliielezea Nowruz kama ishara ya kiangazi na alama ya kuzaliwa upya kwa asili, alielezea matamanio yake kwamba italeta amani, maendeleo, na mustakbali mwema kwa Uturuki, eneo lote, na binadamu wote.
Erdogan alisema aliridhishwa kuona sikukuu ya Nowruz inakuwa ishara ya mwanzo mpya sio tu kwa Uturuki lakini pia kwa majirani.
“Tunakusanyika katika sikukuu ya Nowruz tukiwa na hisia sawa katika mikoa yote 81 na katika ulimwengu wa Turkic," amesema, na kuongeza kuwa Nowruz imetengwa kama siku jumuisha kuzidisha umoja.
Pia amesema kuwa Uturuki itahodhi mkutano wa 13 wa Baraza la Familia mwaka 2026, unaolenga kuongeza kasi.
Erdogan alituma salamu zake kwa “kwa marafiki zetu wote na ndugu zetu kutoka Azerbaijan mpaka Kazakhstan, kutoka Kyrgyzstan mpaka Uzbekistan, kutoka Turkmenistan mpaka Jamhuri ya Uturuki ya Kaskazini mwa Cyprus na Hungary."
“Nawapongeza ndugu zetu wa Syria, Iraq, na ndugu zetu wa Iran, ambao hivi sasa wanapambana na matatizo yaliyosababishwa na vita, katika sikukuu ya Nowruz, na natumai kwamba siku hii muhimu itachangia kumaliza vita katika kanda yetu," amesema.
“Natumai kwamba msimu wa kiangazi ulioletwa na Nowruz utaleta matumaini katika nyoyo zetu, amani katika jamii yetu, na utulivu katika dunia yetu,” ameongeza.
UTURUKI
2 dk kusoma
Rais Erdogan atarajia Nowruz italeta amani Mashariki ya Kati
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan atoa salamu za sikukuu ya Nowruz kwa Syria, Iraq na Iran, akitarajia kwamba siku hiyo itachangia kumaliza migogoro ya kikanda.

Soma zaidi



















