| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Magaidi waua watu kadhaa katika mashambulizi vijijini Nigeria
Msemaji wa polisi anasema vijiji saba viliharibiwa katika mashambulizi hayo ya kundi la kigaidi la Lakurawa.
Magaidi waua watu kadhaa katika mashambulizi vijijini Nigeria
Polisi wanasema vijiji saba viliharibiwa katika mashambulizi hayo. / Reuters
tokea masaa 7

Watu wasiopungua 30 wameuawa siku ya Jumatano katika mashambulizi ya magaidi wanaojulikana kama Lakurawa katika eneo la Arewa kwenye jimbo la Kebbi, polisi walisema siku ya Alhamisi.

Msemaji wa polisi Bashir Usman amesema vijiji saba viliharibiwa katika mashambulizi hayo.

Vyanzo viliiambia Anadolu kuwa washambuliaji hao walienda kutoka kijiji kimoja hadi kingine wakifanya mashambulizi, wakilenga raia kwa makusudi.

Sehemu ya jamii ya Mamunu ilikuwa na idadi kubwa zaidi ya waliouawa 16, vijana watano waliuawa eneo la Awashaka, na wakazi watatu sehemu ya Masama. Jamii zingine zilizoathirika ni Gorin Dena, Kamzo, Dan Mai Rago, na Tungar Bature.

‘Yalikuwa ya kushtukiza’

Wakazi, ambao wengi wao walikimbia katika maeneo ya misitu ya karibu, wanasema hawakutarajia mashambulizi ya kiwango kama hicho. “yalikuwa ya kushtukiza. Walifyatua risasi na kuchoma nyumba,” mwanakijiji mmoja aliiambia Anadolu akitaja asitajwe jina lake.

Kundi la Lakurawa ni la kigaidi linaloendesha mashambulizi yake kaskazini magharibi mwa Nigeria na lina uhusiano na Daesh na ushirikiano na mitandao ya kigaidi ya Mali, Niger, Sokoto na jimbo la Kebbi.

Lakurawa limeibuka kuwa kundi hatari kwa usalama katika miaka ya hivi karibuni, likifanya mashambulizi mabaya kwa jamii za vijijini, kuiba mifugo na kudhibiti kinyume cha sheria baadhi ya maeneo ya kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Machafuko ya hivi karibuni yanakuja huku kukiwa na matatizo ya kiusalama kaskazini magharibi mwa Nigeria, ambapo makundi ya kigaidi yametumia mwanya wa mipaka isiodhibitiwa kushambulia watu, kuiba mifugo na kukabiliana na maafisa wa usalama.

CHANZO:AA
Soma zaidi
Zaidi ya Wakenya 1,000 washiriki katika vita vya Urusi na Ukraine
Guinea-Bissau  yasitisha jaribio la chanjo ya watoto linalofadhiliwa na serikali ya Trump
UNICEF imeonya kuwa kuongezeka kwa ghasia nchini Sudan kunawaweka watoto katika hatari kubwa zaidi
Waziri wa Afya wa Zambia apigwa kalamu katika mabadiliko ya ghafla ya baraza la mawaziri
Ghana yawaondoa raia wake waliojeruhiwa katika shambulio la kigaidi Burkina Faso
Mlipuko wa gesi katika mgodi wa waua watu 38, kujeruhi wengine kadhaa
Namna Uturuki inavyosaidia Rwanda kuwafikia watalii milioni 300 kutoka eneo la Mediterania
Uturuki na Afrika: Safari ya ushirikiano wa muda mrefu na matumaini mapya
Gabon yatangaza kufunga mitandao ya kijamii kwa muda
Nigeria yaonya raia wake dhidi ya kujisajili kupigana vita nje ya nchi
Jesse Jackson, kiongozi wa haki za kiraia nchini Marekani, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84
Somalia kuanza kutoa hati za kusafiria za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Somalia na Tanzania yakubaliana kuhusu ziara bila viza, na kupata viza mtu anapowasili
Wakazi wa Morocco warejea katika mji uliokumbwa na mafuriko
RSF yashambulia hospitali Sudan, na kuwaua watu kadhaa
Tamasha la uvuvi la Argungu latia fora Nigeria
Watu 59 wafariki kufuatia Kimbunga Gezani huku wengine 16000 wakikosa makazi nchini Madagascar
Somalia ilivyofufua jeshi lake kutoka magofu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe
Wanawake barani Afrika katika kutoa muelekeo wa mustakabali wa sayansi
Mgomo wa wafanyakazi wadumaza safari za ndege katika Uwanja Mkuu wa Jomo Kenyatta, Kenya