Siku ya Jumanne Somalia ilishtumu “uvamizi usioruhusiwa” wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gideon Saar eneo la Somaliland, ikitaka Israel “isitishe mara moja” shughuli zozote zinazodunisha uhuru wa Somalia.
Ziara ya Saar ni "uingiliaji usioruhusiwa" wa masuala ya ndani ya taifa huru lililo mwanachama wa Umoja wa Mataifa, taarifa kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje ilisema.
Somalia imesema hatua kama hizo zinakiuka Utaratibu wa Umoja wa Mataifa, Kanuni ya Umoja wa Afrika, na taratibu za uhusiano wa kimataifa, ikiwemo usawa wa uhuru, uhuru wa mipaka, na kutoingilia.
Inasema Somaliland ni “sehemu muhimu na isioganwanyika” ya Somalia.
Somalia inasema kuwa ziara yoyote rasmi, mawasiliano, au majadiliano katika maeneo yake bila kuhusisha serikali kuu hairuhusiwi, batili, na haina msingi wowote kisheria.
Wizara imetaka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu, Ushirikiano wa Mataifa ya Kiislamu, na washirika wengine wa kimataifa kuthibitisha uhuru wa Somalia na mipaka yake inayotambulika kimataifa “waziwazi bila kusita.”
“Somalia ina haki ya kuchukua hatua stahiki za kidiplomasia na kisheria, kulingana na sheria ya kimataifa, kulinda uhuru wake, umoja wa taifa, na uhuru wa nchi,” ilisema.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gideon Saar aliwasili eneo lililojitenga la Somalia, Somaliland siku ya Jumanne, karibu wiki mbili baada ya Israel kutambua eneo hilo huku jamii ya kimataifa ikishtumu hatua hiyo, kulingana na taarifa za vyombo vya habari.
Disemba 26, Israel ilitangaza kutambua rasmi Somaliland kama huru, taifa huru, kufanya Israel kuwa nchi pekee duniani kutambua eneo hilo lililojitenga.
Hatua hiyo ya Israel ilishtumiwa kote katika kanda, hasa kutoka nchi za Kiarabu, ambazo ziliilezea kama isiyo halali na tishio kwa amani na usalama kimataifa.
Somalia pia imethibitisha dhamira yake ya msingi kuhusu uhuru wake, umoja wa taifa, na kukataa hatua hiyo ya Israel.
Somaliland, ambayo haijtambuliwa rasmi tangu kutangaza uhuru wake kutoka kwa Somalia 1991, inajisimamia yenyewe kiutawala, kisiasa, na kiusalama, huku serikali kuu ikishindwa kuonesha uwezo wake katika eneo hilo, na uongozi wake kushindwa kutambuliwa kwa uhuru kimataifa.





















