Maoni
ULIMWENGU
3 dk kusoma
Kumbukumbu za Oktoba 7: kinachokumbukwa na matokeo yake kufikia sasa
Miaka miwili baadaye, matukio ya Oktoba 7 bado ni tata. Simulizi inayojitokeza inategemea tafisri ya matukio, namna dunia inavyoitizama Israel, Palestina, na uwezekano wa kupatikana kwa amani iliyo tete.
Kumbukumbu za Oktoba 7: kinachokumbukwa na matokeo yake kufikia sasa
Utata kuhusu namna gani ya kukumbuka matukio ya Oktoba 7 unaendelea kuwa na maoni tofauti kuhusu Israel, Palestina / AP
8 Oktoba 2025

Oktoba 7, 2023, ni siku ambayo maana yake na athari zake zinatengeneza msingi wa namna matukio ya miaka miwili iliyopita yalivyokuwa, na namna gani matukio hayo yanavyoshawishi yanayoendelea sasa.

Tukio hilo bado ni tata, kuna maswali mengi, na ukweli ambao bado haujathibitishwa:

Mashambulizi hayo yakionekana kama tukio la mapambano ya Palestina, kwa Israel kushindwa kuheshimu matokeo ya ushindi wa
Hamas katika uchaguzi 2006 uliokuwa na waangalizi wa kimataifa?

Au mashambulizi hayo ni majibu ya kuishi katika mazingira ya udhalimu chini ya sera za ubaguzi za kukandamizwa?

Au Okotoba 7 inakumbukwa kama mashambulizi yaliyoyotokea bila kuchokozwa na kudhihirisha “ukatili wa Hamas” na hasa watu wote wa Palestina wa Gaza, kama alivyotangaza Rais wa Israel,
Isaac Herzog?

Au Israel ilionywa na kuruhusu mashambulizi hayo kutokea ili kutimiza mpango wa kizayuni wa
‘Israel Kubwa’ kwa kupanua maeneo ya Israel hadi katika maeneo ya Palestina ya Gaza, na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, na Jerusaleme Mashariki, na katika mchakato huo kumaliza kabisa ndoto za kuwepo kwa taifa la Palestina?

Au, kwa uwazi kabisa, namna Israel ilivyojibu mashambulizi ya Oktoba 7 ilikuwa ni mpango wa mauaji ya halaiki, ambayo yalidhihirisha kuhusika kwa nchi zenye demokrasia huru za bara Ulaya na Marekani Kaskazini na udhaifu wa wa sheria ya Kimataifa na Umoja wa Mataifa kuhusu kutekeleza sheria na uwajibikaji kwa wanaofanya makosa?

Badala ya taharuki kati ya wale wanaounga mkono na wale wanaopinga Israel, watu wanaangazia zaidi matokeo ya kidiplomasia ambayo yatasaidia kusitishwa kwa mapigano, kubadilishana wafungwa, na uhakika wa kutokuwajibisha waliofanya makosa kutoka pande zote mbili.

Hatua I: Miezi baada ya Oktoba 7 - Israel iko kwenye ati ati

Licha ya viongozi wa Israel, ikiwemo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na waziri wa zamani wa Ulinzi Yoav Gallant, kutumia lugha ya mauaji ya halaiki katika majibu yao ya awali kwa mashambulizi, neno ‘mauaji ya halaiki’ ilikuwa ni mwiko kueleza hatua za Israel. 

Hatua II: Maamuzi ya ICJ/ICC na kura ya turufu kwa kusitishwa mapigano   

Wasiwasi wa jamii ya kimataifa ulianza kuangazia matatizo kwa watu wa Gaza na madhila wanayopitia Wapalestina, pamoja na ukatili na kukosekana kwa hakikisho kuwa mashambulizi ya Israel yalihusiana na wasiwasi wa kweli kuhusu usalama.

Hatua III: Ripoti ya Pillay, diplomasia ya Trump, na mpango wa baada ya Oktoba 7

Mambo mengi yametokea na kudhihirisha mauaji ya halaiki 2025, huku matukio ya Oktoba 7 kwa sehemu fulani yakisahaulika.

Tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa
iliongozwa na Kamishna Mkuu wa zamani Navi Pillay ilikamilisha ripoti yake katikati mwaka 2025 kuwa mashambulizi ya Israel huko Gaza ni mauaji ya halaiki, ikiwa ni sawa na ripoti zingine tatu za Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa Francesca Albanese kupunguza kasi ya mradi wa walowezi wa kikoloni wa Israel na njia ya kusitisha mauaji ya halaiki.

Pamoja na kuwa mabadiliko mengi yametokea tangu Oktoba 7, 2023, katika matukio yote ya Israel/Palestina, kuna masuala manne ambayo yatakuwa tatizo katika miaka miwili ijayo: Marekani kuunga mkono Israel bila kutumia busara, kuitenga Palestina kutopata uwakilishi na kuwanyima haki ya kuwa na taifa lao wenyewe, kwamba Hamas waendelee kutambuliwa kama magaidi, na kuwakandamiza Wapalestina kwa kutumia itikadi ya Kizayuni na mifumo ya kibaguzi ya utawala wa Israel.

Ni pale tu ambapo mabadiliko ya kweli yatakapofanyika katika masuala haya na tafsiri sahihi ya matukio ya Oktoba 7 itakapofanyika ndiyo heshima itabainika.

CHANZO:TRT World