| swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Wakenya zaidi ya 200 wajiunga na jeshi la Urusi
Serikali ya Kenya imesema zaidi ya raia wake 200 wamejiunga na jeshi la Urusi katika vita vinayvoendelea kati ya Urusi na Ukraine, na kwamba mashirika ya ajira bado yanaendelea kutafuta Wakenya zaidi kujiunga katika mapigano.
Wakenya zaidi ya 200 wajiunga na jeshi la Urusi
Ukraine ilisema kuwa zaidi ya raia 1,400 kutoka nchi zipatazo thelathini za Afrika wanapigana upande wa Urusi. /
13 Novemba 2025

Wiki iliyopita, Ukraine ilisema kuwa zaidi ya raia 1,400 kutoka nchi zipatazo thelathini za Afrika wanapigana upande wa Urusi nchini humo, baadhi yao wakiwa wameajiriwa kwa kuhadaiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andriy Sybiha, alisema Urusi inawashawishi Waafrika kusaini mikataba ambayo ni “sawa na hukumu ya kifo,” na akazitaka serikali za Afrika kuwaonya raia wao.

“Shughuli za uajiri nchini Urusi zinaripotiwa kupanuka na sasa zinawahusisha pia raia wa Kiafrika, wakiwemo Wakenya,” ilisema taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya.

Hata hivyo Ubalozi wa Urusi jijini Nairobi haukutoa ufafanuzi kuhusu hilo.

Kulingana na wizara hiyo, ubalozi wa Kenya mjini Moscow umerekodi majeraha miongoni mwa baadhi ya waajiriwa, ambao inadaiwa waliahidiwa hadi dola 18,000 ili kulipia gharama za visa, usafiri na makazi.

Msako wa usalama uliotekelezwa karibu na Nairobi mnamo Septemba uliwaokoa Wakenya 21 ambao, wizara ilisema, walikuwa wakitayarishwa kutumwa vitani. Mtu mmoja alikamatwa na anakabiliwa na mashtaka kuhusiana na tukio hilo.

Wizara hiyo ilisema kwamba waliookolewa walikuwa wamepotoshwa kuhusu aina ya kazi yao, ikiamini kuwa waliajiriwa kwa majukumu yasiyo ya vita kama vile kuunganisha ndege zisizo na rubani, na upigaji rangi.

CHANZO:Reuters
Soma zaidi
Cape Verde, Mauritius na Ushelisheli wafanikiwa kuangamiza surua na  rubela
Rais wa Sudan Kusini Kiir amrejesha makamu wa rais katika mabadiliko ya baraza la mawaziri
Zaidi ya watu 100,000 wamekimbia makazi yao kutoka Al Fasher ya Sudan tangu kutwaliwa na RSF
Rais wa Tanzania amteua binti na mkwe wake katika Baraza la Mawaziri
Rais Samia amteua waziri mpya wa fedha, awaacha mawaziri wa mambo ya nje na madini madarakani
Tovuti za taasisi za serikali ya Kenya zashambuliwa
Mgodi waporomoka DRC na kuua watu wasiopungua 32
Wahamiaji 4 wafariki baada ya boti mbili zilizokuwa zimebeba makumi ya watu kuzama pwani ya Libya
Kikundi cha matabibu kinaripoti visa ya ubakaji wa wasichana wa Al Fasher baada ya RSF kuteka
Mlipuko wa virusi vya Marburg umethibitishwa kusini mwa Ethiopia
DR Congo, M23 wasaini makubaliano ya amani 'ya kihistoria' nchini Qatar
Baraza la Maaskofu Tanzania lataka uwajibikaji kwa waliohusika na mauaji ya waandamanaji
Baraza la usalama la UN laongezea mwaka mmoja ujumbe wa amani wa Abyei
Kiongozi wa zamani wa waasi wa DRC anayeshtakiwa Paris kwa uhalifu wa kivita aanza mgomo wa kula
UN yaagiza uchunguzi wa dharura ufanyike kuhusu ukiukaji wa sheria katika Al Fasher ya Sudan
Rais wa Tanzania atangaza uchunguzi kuhusu mauaji ya waandamanaji katika uchaguzi
Wakimbizi 57,000 wamewasili kaskazini mwa Sudan baada ya mashambulizi ya RSF huko Darfur, Kordofan
Afrika Kusini yaruhusu kuingia kwa wakimbizi zaidi ya 150 kutoka Gaza, Palestina
Afrika yakumbwa na mlipuko wa kipindupindu mbaya zaidi katika miaka 25
Mataifa ya G7 walaani mashambulizi ya RSF dhidi ya raia Sudan, watoa wito wa kusitishwa mapigano