| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Kenya Airways yafaidika kifedha kutokana na vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati
Shirika la ndege la Kenya Airways limesema kuwa idadi ya wateja wake imeongezeka kwa kiasi kikubwa kufuatia athari za vita vinavyoendelea katika Mashariki ya Kati, ongezeko kubwa likitokana na wasafiri kutoka Ulaya, Marekani na Asia.
Kenya Airways yafaidika kifedha kutokana na vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati
Shirika la ndege la Kenya Airways linasema mahitaji ya viti katika safari zake yalikuwa karibu 100% kufikia Machi 2026. / / Reuters
tokea masaa 3

Shirika la ndege la Kenya Airways limetangaza siku ya Jumatatu kuwa idadi ya wateja wake immeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na vita vinavyoendelea katika Mashariki ya Kati. Ongezeko hili limeonekana hasa kwa wasafiri kutoka Ulaya, Marekani, na Asia.

Vita vinavyohusisha Marekani, Israel, na Iran vimevuruga sekta ya usafiri wa anga duniani. Matokeo yake, baadhi ya mashirika ya ndege yamepandisha nauli, kubadilisha ratiba za safari ili kuepuka viwanja vya ndege vya Mashariki ya Kati, au hata kufuta baadhi ya safari.

Kenya Airways imeripoti kuwa kiwango cha ujazo wa viti kwenye ndege zake kimepanda kutoka takriban asilimia 70 mwezi Januari hadi kufikia karibu asilimia 100 hivi sasa. Hii inaonyesha ndege nyingi sasa zinajazwa kwa kiasi kikubwa, jambo linaloongeza mapato ya shirika.

"Tulikuwa na kiwango cha chini hadi Februari, kisha ukaongezeka kwa kasi kubwa. Tulifikia 90%, na hata 99% kwa baadhi ya safari," alisema George Kamal, kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kenya Airways.

Siku hamsini na sita za usambazaji wa mafuta ya ndege

Aliongeza kuwa ongezeko kubwa limechangiwa na wasafiri kutoka Ulaya, Marekani, na Asia, na safari hizi zinaongeza faida kwa mtandao wa shirika.

Kwa upande wa usambazaji wa mafuta ya ndege, Kenya Airways ina takriban siku 56 za akiba, na shirika linafanya juhudi za kuongeza usambazaji kutoka India, alisema Paul Njoroge, mkuu wa uendeshaji wa safari za ndege.

CHANZO:Reuters