| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Dabi ya Manchester Ligi Kuu ya England
Kaimu meneja wa Manchester United Michael Carrick ataiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza Jumamosi wakati wa dabi ya Manchester uwanjani Old Trafford.
Dabi ya Manchester Ligi Kuu ya England
Kaimu meneja wa Manchester United Michael Carrick. / Reuters
16 Januari 2026

Kaimu meneja wa Manchester United Michael Carrick ana kibarua kikubwa cha kurudisha imani kwa mashabiki wa timu hiyo ambayo Jumamosi inacheza katika dabi ya Manchester ikiwa uwanja wa nyumbani.

United wako nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England wakiwa wameshinda mechi moja katika sita zilizopita kwenye ligi hiyo na wiki iliopita walitolewa kwenye mashindano ya Kombe la FA.

Hii itakuwa fursa ya kwanza kwa Carrick kuona kama atampiku Pep Guardiola, ambaye timu yake Manchester City iko katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi ikiwa alama sita nyuma ya Arsenal, licha ya kupata sare tatu mfululizo.

Kwingineko mwishoni mwa wiki, Arsenal wanaoongoza jedwali la Ligi watacheza dhidi ya Nottingham Forest iliyo nafasi ya 17.

Liverpool itakuwa wenyeji wa Burnley Jumamosi. Vijana hao wa Arne Slot anbayo ndiyo mabingwa wa sasa wako nafasi nne katika msimamo, alama 14 nyuma ya Arsenal. Burnley wako kwenye nafasi tete ya kushuka daraja ya 19.

CHANZO:TRT Afrika Swahili