Gabon ni taifa la Afrika ya Kati lililoko mwisho wa magharibi wa msitu wa mvua wa Bonde la Congo, unaosemekana kuwa msitu wa pili wa mvua duniani.
Inaripotiwa kuwa na takriban hekta milioni 22 za misitu ya mvua ya kitropiki huku zaidi ya 88% ya eneo lake lote likifunikwa na misitu ya mvua.
Sehemu kubwa ya ardhi yenye misitu ni chanzo cha kupatikana kwa chakula, dawa, nishati, na njia ya mapato na maisha kwa mamilioni ya watu katika eneo la Bonde la Congo, ambalo ni la pili kwa ukubwa baada ya msitu wa Amazon ulioko Brazil.
Misitu ya Gabon ni makazi ya wanyamapori na mimea mikubwa mikubwa aina tofauti, ikiwa ni pamoja na 60% ya tembo wa misitu ambao wako hatarini kuangamia.
Tembo hawa wanaojulikana kwa majukumu yao katika kusaidia mazingira wanajulikana kuwa na: uwezo wa kuchimba na kuvuna.
Misitu hii pia ina idadi kubwa ya sokwe wa nyanda za chini za magharibi, kima aina ya "mandrill", nyati wa msituni, na aina tofauti ya ndege maarufu.
Misitu hapa pia inachukua jumla ya tani milioni 140 za gesi ya kaboni dioksidi kila mwaka.
Tangu mwaka 2000 Gabon imehifadhi sehemu kubwa ya msitu wake wa mvua, na kufanikisha kuwa na hifadhi za taifa 13, mojawapo imeorodheshwa kwenye Tovuti ya shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Urithi wa utamaduni, UNESCO.
Msitu wote wa Gabon ni mali ya serikali lakini mashirika binafsi yamepewa fursa ya kusimamia misitu hiyo.
Jukumu la kulinda utajiri huu ni la serikali moja kwa moja huku kukiwa na hifadhi 13, ambazo yanachangia takriban 12% ya mapato ya taifa.
Halafu kuna eneo la vijijini kwa ujumla ambapo ardhi na misitu inatumika na jamii za wakaazi wa maeneo hayo, na wako hutu kufanya shughuli zao za kijadi, ikiwa wanazingatia miongozio iliyowekwa na wasimamizi wa hifadhi wa serikali.
90% ya miti maarufu ulimwenguni inayojulikana kama okoume, inatoka katika misitu ya Gabon. Miti hii hutumika katika kutengeneza mbao bora, na miti migumu kama mikangazi.
Miti aina ya Keva Zingo pia hutumika katika kutengeneza mbao ngumu na nzito na pamoja na miti ya mpingo(ebony trees).
Miti mingine ni dibetou maarufu kama tigerwood, movingui au satinwood ya Nigeria, na zingana maarufu zebrawood.
Ingawa viwango vya ukataji miti viko chini nchini Gabon, baadhi ya mambo yanayochochea ukataji miti ni pamoja na kushindwa kupanua wigo wa kilimo, ukataji wa mbao kwa ajili ya kuni, na kuimarisha miundombinu.














