| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Biashara ya Uturuki-EU yafika Dola Bilioni 233 huku majadiliano ya Umoja wa Forodha yakiimarishwa
Majadiliano yanahusisha kuangazia biashara kwa njia ya elektroniki, manunuzi, uwekezaji na kilimo.
Biashara ya Uturuki-EU yafika Dola Bilioni 233 huku majadiliano ya Umoja wa Forodha yakiimarishwa
Waziri wa Biashara Omer Bolat anasema amefanya rasmi mara tatu mjini Brussels katika kipindi cha miezi mitatu iliopita. / Anadolu Agency

Uturuki na Umoja wa Ulaya wanapiga hatua katika majadiliano kuhusu Umoja wa Forodha, huku mazungumzo ya watalaamu yakiangazia biashara kwa njia ya elektroniki, manunuzi ya umma, uwekezaji na bidhaa za kilimo, waziri wa biashara wa Uturuki Omer Bolat alisema.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara jijini Brussels, Bolat anasema majadiliano yalikuwa yanaangazia “hatua kwa hatua”, licha ya Baraza la EU kutoidhinisha kuanzishwa kwa mazungumzo ya mfumo wa kisasa wa Umoja wa Ulaya.

Alisema mazungumzo ya kitaalamu na wenzao wa Ulaya tayari yanaendelea, kufuatia kumalizika kwa tathmini ya pande zote mbili na kuidhinishwa kwa sheria mpya ya manunuzi ya umma na Uturuki mwishoni mwa mwezi Julai.

“Tunapiga hatua kwa masuala mbali mbali tangu masuala husika kujitokeza na mamlaka ya Tume ya Ulaya zinafanya majadiliano na sisi,” Bolat alisema.

Alisisitiza kuwa kuendeleza uhusiano wa kiuchumi ni muhimu kwa EU kutokana na kuwa Uturuki, akieleza biashara kati ya pande hizo mbili imeongezeka mara kumi na moja zaidi katika kipindi cha miongo mitatu iliopita na kufikia Dola Bilioni 233.

Biashara ya viwanda na kidijitali

Bolat anasema mwaka uliopita Uturuki imekuwa ikiangazia changamoto za vipengele kuhusu Sheria ya IAA.

Alionya kuwa baadhi ya hatua kwenye muswada huo zinaweza kuathiri mustakabali wa uwekezaji na kutatiza mfumo wa ugavi, hasa kuhusu magari ya umeme na sekta ya magari.

Uturuki inasisitiza kuwa mawasiliano na maafisa wa EU kueleza matarajio yao na kupunguza uwezekano wa athari za kiuchumi kutokana na sheria zilizopendekezwa, aliongeza.

Bolat pia alisema Umoja wa Ulaya unashirikiana na Uturuki kuhusu maandalizi ya sheria kuhusu biashara ya kidijitali. Uturuki haiathiriwi na sheria mpya ya utaratibu wa EU kuweka tozo la Euro 3 kwa kila mzigo, alisema.

Alionya kuwa uingiliwaji wa kisiasa na Bunge la Ulaya kunaweza kuwa na athari mbaya, akiongeza kuwa maafisa wengi wa Ulaya pia wanaunga mkono Uturuki katika mpango wa asili wa “Made in EU”.

Hata hivyo, alieleza kuwa EU inajumuisha nchi ambazo zina maslahi tofauti ya kiuchumi, akitoa wito wa mtazamo “wa utulivu na makini”.

Bolat alisema kuwa amefanya ziara tatu rasmi mjini Brussels katika kipindi cha miezi mitatu iliopita, ikiwa alifanya ziara kama hizo mara tano mwaka uliopita, na kueleza matumaini ya kupigwa kwa hatua katika mazungumzo.

Soma zaidi
Uturuki inalaani vikali shambulio la wanamgambo wa Houthi katika uwanja wa ndege Riyadh
Uturuki yapiga marufuku majukwaa ya mitandao ya kijamii kuwahudumia watoto walio chini ya miaka 15
Selcuk Bayraktar aonya kuwa mbio za teknolojia zisizodhibitiwa zinaweza kusababisha 'angamizo
Erdogan: Mikataba ya kimataifa “imepoteza ufanisi wake”
TRNC yashtumu EU kwa kuendeleza 'msimamo usio wa haki' wa kuitenga Kupro ya Uturuki
Mkataba wa Makkah hautoi uhalali wa kushambulia mataifa mengine, asema Fidan
Chuo cha METU cha Uturuki kupeleka kigari kidogo mwezini 2030
Trump azipongeza Uturuki na Pakistan kwa kuipa Saudi Arabia msaada wa kijeshi
Erdogan na Putin wajadili usalama wa Bahari Nyeusi na masuala ya Urusi na Ukraine
Waziri Mkuu wa Canada kuitembelea Uturuki
Erdogan: Uturuki haitorudi nyuma kwenye mradi wake wa anga za mbali
Uturuki na washirika wake wakubaliana kuupa nguvu mkataba wa Makkah dhidi ya mashambulizi ya Wahouth
Uturuki inabadilisha sekta ya ulinzi kwa 'mageuzi kamili': Erdogan
Uturuki yaadhimisha Siku ya Ushirikiano wa Mataifa ya Kituruki
Uturuki yalaani shambulio la Wa-Houthi dhidi ya miundombinu ya Msikiti wa Mtume
Uturuki kuikabidhi Iraq hatua kwa hatua kambi ya Bashiqa-Zilkan: Wizara ya Ulinzi
Maonesho ya teknolojia ya anga Teknofest yaanza nchini Uturuki
Emine wa Uturuki aongoza wito wa kimataifa wa kuweka mfumo wa UN wa kulinda watoto mtandaoni
Erdogan: Uturuki itaendelea kuzungumza kwa ajili ya Wapalestina
Erdogan, Prabowo wamejadili uhusiano wa Uturuki na Indonesia, masuala ya kikanda