| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Afrika Magharibi na Kasi ya Kusafisha Dhahabu
Wataalamu wanasema mafanikio yatategemea zaidi ya kujenga viwanda vya kusafisha dhahabu. Nchi zinahitaji vifaa vya dhahabu vya kuaminika, umeme wa bei nafuu, mifumo ya ununuzi wa uwazi na ufikiaji wa masoko ya kimataifa.
Afrika Magharibi na Kasi ya Kusafisha Dhahabu
Nchi za Afrika Magharibi ni miongoni mwa wazalishaji wakuu wa dhahabu duniani / Reuters (Wire)

Nchi za Afrika Magharibi ni miongoni mwa wazalishaji wakuu wa dhahabu duniani.

Hata hivyo, dhahabu yao nyingi inasafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kusafishwa.

Sasa, serikali zinatafuta namna ya kubadilisha hali hiyo  kwa kuwekeza katika viwanda vya ndani vya kusafisha, kuimarisha kanuni za usafirishaji nje na kuchukua udhibiti mkubwa wa mnyororo wa uongezaji thamani ya dhahabu.

Burkina Faso ilifungua kiwanda chake cha kwanza cha kusafisha dhahabu, Raffinor-BF, mwaka 2026, kikiwa na uwezo wa awali wa tani 164 kila mwaka na inapanga kupanua hadi tani 515.

Guinea pia imezindua Kiwanda chake cha Kusafisha Dhahabu cha Nimba, chenye uwezo wa kusindika tani 530 kila mwaka, huku Ghana tayari ikiwa na viwanda kadhaa.

Wakati huo huo, Mali inaendeleza kiwanda cha kusafisha tani 200 kwa mwaka.

Uwekezaji huu unalenga kuleta ajira, kutoa mapato ya ziada na kupunguza utegemezi wa vifaa vya kusafisha nje.

Hata hivyo, wataalamu wanasema kuwa na viwanda haitoshi.

Hofu kubwa ni kwamba Afrika Magharibi inaweza kuwa na uwezo mkubwa wa kusafisha kuliko dhahabu inayozalisha.

Uwezo wa pamoja uliotangazwa au ulioagizwa nchini Ghana, Guinea, Burkina Faso na Mali unazidi tani 1,000 kila mwaka, ikilinganishwa na makadirio ya uwezo wa uzalishaji wa kikanda wa takriban tani 585.

Hili linazua maswali kuhusu iwapo viwanda vya kusafisha dhahabu vinaweza kupata dhahabu ya kutosha kufanya kazi kwa faida.

Changamoto nyengine ni pamoja na faida ndogo katika kusafisha dhahabu, kufikia viwango vya kimataifa vya uidhinishaji, na kukabiliana na uchimbaji haramu na magendo.

Guinea tayari imepitia wakati mgumu baada ya kuzuia mauzo ya nje ya dhahabu isiyosafishwa, huku baadhi ya makampuni ya uchimbaji madini yakikabiliwa na ucheleweshaji wakati mipango ya kusafisha dhahabu ya ndani ilipoanzishwa.

Hatimaye, wataalamu wanasema mafanikio yatategemea zaidi ya kujenga viwanda vya kusafisha dhahabu.

Nchi zinahitaji vifaa vya dhahabu vya kuaminika, umeme wa bei nafuu, mifumo ya ununuzi wa uwazi na ufikiaji wa masoko ya kimataifa.

Kwa wataalamu wa Afrika magharibi wanasema jaribio halisi ni kama uwekezaji huu katika sekta ya dhahabu unaweza kujenga viwanda endelevu, kuzalisha mapato zaidi na kuhakikisha kwamba faida kubwa zinafikia nchi na jamii zinazozalisha dhahabu hiyo

CHANZO:Reuters (Wire)