| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance aghairi ziara iliyopangwa nchini Kenya
Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance amesitisha ziara yake nchini Kenya iliyopangwa kufanyika baadaye mwezi huu baada ya safari yake aliyotarajia kwenda kwenye mkutano wa G20 nchini Afrika Kusini kufutwa na Rais Donald Trump.
Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance aghairi ziara iliyopangwa nchini Kenya
Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance alikuwa amepanga kuzuru Kenya baada ya mkutano wa G20 nchini Afrika Kusini baadaye mwezi wa Novemba. / Picha: AP / AP
11 Novemba 2025

Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance ameghairi ziara yake nchini Kenya iliyopangwa mwishoni mwa mwezi huu baada ya safari yake iliyotarajiwa kwenye mkutano wa G20 Afrika Kusini kuahirishwa na Rais Donald Trump, serikali ya taifa hilo la Afrika Mashariki ilisema Jumatatu.

Vance alikuwa amepanga kutembelea Kenya baada ya kuhudhuria mkutano wa Kundi la Mataifa 20 (G20) huko Afrika Kusini kuanzia Novemba 22 hadi 23.

Lakini Trump alisema Ijumaa kwamba hakuna maafisa wa Marekani watakaohudhuria G20, akidai ukiukaji wa haki za binadamu uliofanywa na Afrika Kusini dhidi ya jamii ndogo ya Wafirikaner wa rangi nyeupe, madai ambayo Afrika Kusini imeyakataa mara kwa mara.

Kutokana na uamuzi wa Trump, Kenya imelipokea taarifa kwamba ziara ya Vance nchini Kenya pia imeghairiwa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya ilisema katika taarifa.

Mshirika mkuu asiokuwa wa NATO

Kenya imesema inataka kufikia makubaliano ya kibiashara na Marekani kufikia mwisho wa mwaka huu. Taarifa yake ilisema kwamba kufutwa kwa ziara ya Vance "hakuathiri uhusiano imara na wa kudumu kati ya mataifa yetu mawili."

Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden alimteua Kenya kuwa mshirika mkuu asiokuwa wa NATO mwaka 2024, lakini Nairobi imekabiliwa na ukosoaji kutoka kwa wabunge wa Marekani miezi ya hivi karibuni kuhusu hatua za kuimarisha uhusiano na China.

CHANZO:Reuters