| Swahili
Maoni
AFRIKA
3 dk kusoma
Vita vya Sahel na changamoto za makundi ya kigaidi
Mamilioni ya watu wanashambuliwa na magaidi wakiweka aina fulani ya utaratibu, mataifa ya Sahel yanajitahidi kudhihirisha kuwa katika nchi zao, ndiyo wadhamini halisi wa raia, wala siyo mtutu wa bunduki.
Vita vya Sahel na changamoto za makundi ya kigaidi
Kundi la kigaidi lenye uhusiano na Al Qaeda-JNIM na Daesh-GS wanaendeleza uwepo wao eneo la Sahel. / AFP
5 Januari 2026

Na Göktuğ Çalışkan

Huku 2026 ikianza, eneo la Sahel halikabiliani tena na magaidi wanaotoka kwenye jangwa na kushambulia msafara wa magari na kukimbia, mtazamo wa vita umebadilika, kiharakati, na kimkakati.

Katika eneo la Liptako-Gourma, Muungano wa Mataifa ya Sahel (AES) unakabiliana na tatizo ambalo ni changamoto ambayo siyo tu changamoto kwa taifa, bali lina lengo na kuliondoa taifa.

Mustakbali wa eneo hilo unapatiwa ufumbuzi kwa vita vya nani anatakiwa kuwa uongozini, uwezo, na huduma zinazotolewa.

Kwa upande mwingine, makundi ya kigaidi kama yale yenye uhusiano na Al Qaeda-JNIM na Daesh-GS, yanaendeleza ubabe wake, kwa kuweka hofu, kuweka vizuizi barabarani, na mifumo ya kuamiliana na watu.

Kujidanganya kuhusu mkakati

Tathmini nyingi ya kutoka nje inaonyesha kwa makosa kuwa maeneo ambayo serikali ya Mali au Burkina Faso yanashindwa kufika ni kama "maeneo yasiyoweza kutawaliwa."

Katika maeneo mengi ya vijijini, kundi la kigaidi la JNIM limetekeleza mfumo mbadala wa uongozi.

Wana mahakama za muda ambazo zinatatua masuala ya ardhi kwa mafanikio na migogoro mingine kati ya wakulima na wafugaji. Ndani ya saa chache, wanatatua, yale ambayo mamlaka za serikali zinaona kama hayawezekani, na yangechukuwa muda wa miezi kadhaa kutatua.

Makundi yenye silaha yanaonekana kama ndiyo yenye "ufumbuzi" wakati taifa linaonekana kama "halipo."

Ukusanyaji wa kodi pia unamaasha utawala. Kile ambacho kinaonekana kama kurubuniwa kinaleta usalama katika maeneo mengine, na kuwa na mfumo mahsusi, pamoja na ahadi ya kupata ulinzi. Ujumbe uko wazi: serikali inakusanya bila kutoa ahadi zozote za msaada; makundi hayo yanakusanya yakiahidi kuwapa usalama.

Silaha ya njaa

Utawala huu wa kutumia silaha una changamoto zake: kuzuia njia, ikiwa ni paoja na kufunga barabara, masoko, na vivuko,kusababisha matatizo zaidi kwa watu. Lengo ni kutatiza umoja wa watu, na kufanya wategemee makundi hayo kwa ajili ya maisha yao.

Hali hii inatumika kama mkakati wa kisiasa: kudhoofisha mataifa, alafu kupendekeza ‘‘kuwekwa kwa utaratibu" na watu wote wawe chini ya utawala wao.

Kuelekea kuwa na umoja wa Sahel

Wakati tukianza mwaka 2026, hali si mbaya sana. Jamii bado haiamini uongozi.

Changamoto ya mamlaka za mpito za Mali, Burkina Faso, na Niger ni namna ya kubadilisha imani ya watu ili wawe watiifu kwao, na baadaye kufanya liwe suala endelevu kwa uwezo wa taifa.

Makundi yenye silaha yanataka kuwa na taifa mbadala kwa serikali ambayo inaonekana haiko karibu na watu wake. Hili haliwezi kufanyika kirahisi na kurudisha hali ilivyokuwa zamani.

Kilicho hapa vita vya Sahel ni kwa ajili ya utawala bora: vita ambavyo uraia na usalama haviwezi kutenganishwa, na ambapo ushindi utapimwa kwa uwezo wa kudhibiti maeneo, na baadaye kuunganisha jamii pamoja.

Mwandishi, Göktuğ Çalışkan, ni mwanafunzi wa shahada ya uzamifu (PhD) na mtaalamu wa Uhusiano wa Kimataifa.

Kanusho: Maoni ya mwandishi hayawakilishi mtazamo, maoni na sera za uhariri za TRT Afrika.


CHANZO:TRT Afrika