| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Washukiwa wa ugaidi washambulia mgodi wa dhahabu, wawateka wafanyakazi nchini Mali
Washukiwa wa ugaidi wameshambulia mgodi wa dhahau wa Morila nchini Mali mwishoni mwa wiki, kuchoma vifaa na kuwateka wafanyakazi saba kabla ya kuwaachilia baadaye, afisa mmoja kutoka kwa wizara ya madini ameiambia Reuters Jumatatu.
Washukiwa wa ugaidi washambulia mgodi wa dhahabu, wawateka wafanyakazi nchini Mali
Mashambulizi ya hivi karibuni yanadhihirisha hatari ya usalama inayoongezeka nchini Mali. / Reuters
5 Januari 2026

Washukiwa wa ugaidi wameshambulia mgodi wa dhahabu wa Morila nchini Mali mwishoni mwa wiki, kuchoma vifaa na kuwateka wafanyakazi saba kabla ya kuwaachilia baadaye, afisa mmoja wa wizara ya madini aliaambia Reuters Jumatatu.

Mashambulizi hayo yanaonesha hatari ya usalama inayoongezeka nchini Mali, mzalishaji mkubwa wa tatu wa dhahabu barani Afrika, ambayo inakabiliana na magaidi wenye uhusiano na al Qaeda waliolenga uwekezaji wa kigeni na raslimali zingine.

Siku ya Jumamosi, watu waliokuwa na silaha walivamia mgodi, ambapo kampuni yenye makao yake Marekani Flagship Gold ilitia saini ya uwekezaji mwaka uliopita, msemaji wa wizara ya madini na mtu mwingine anayefahamu kuhusu hilo alisema.

Walichoma vifaa na kuwateka wafanyakazi saba, lakini waliwaachilia siku ya pili jioni, vyanzo hivyo vilisema. Wote waliomba majina yao yasitambulishwe.

'Hali imedhibitiwa'

Kampuni ya Flagship Gold haikutoa taarifa haraka kuhusu hilo ilipoombwa kuzungumzia suala hilo.

Msemaji wa wizara anasema kuwa jeshi sasa limechukuwa udhibiti na linafanya msako katika eneo hilo.

Kampuni hiyo yenye makao yake jijini New York ya Flagship Gold, ambayo ilisajiliwa mwezi Juni 2024, ilitia saini ushirikiano wa makubaliano na kampuni ya madini ya serikali ya Mali mwezi Oktoba kuanza uchimbaji madini katika mgodi wa dhahabu wa Morila.

Mgodi huo ulioko katika kanda ya kusini ya Mali ya Sikasso, una zaidi ya tani 70 za dhahabu, kulingana na wizara ya madini.

Ulichukuliwa na serikali baada ya kampuni ya Australia Firefinch kuacha kuchimba kutokana na uzalishaji mdogo na gharama kubwa za uchimbaji. Zamani mgodi wa Morila ulikuwa ukichimbwa na Barrick na AngloGold Ashanti.

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
Jeshi la Benin lawaua 'magaidi' 45 kaskazini mwa nchi
Nchi za Afrika zaunga mkono Venezuela baada ya operesheni ya kijeshi ya Marekani iliyomlenga Maduro
Somalia yashtumu ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Israel Somaliland, ikiitaja kama ‘uvamizi’
Mahakama ya Tunisia yawaachilia huru wafanyakazi wa NGO waliokamatwa kwa kuwasaidia wahamiaji
Baraza la Makanisa nchini Kenya lajitenga na mhubiri anayedai miujiza 'Nabii Owour'
Misri imepokea watalii milioni 19 mwaka 2025: Waziri
Rais Touadera achaguliwa tena kuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
Vita vya Sahel na changamoto za makundi ya kigaidi
Tanzania yapiga marufuku wageni kutoa baadhi ya huduma katika sekta ya madini, kulinda wazawa
Mahakama Kuu ya Guinea yamthibitisha Doumbouya mshindi wa uchaguzi
Jeshi la Sudan lazuia shambulio la droni la RSF kwenye bwawa kuu na maeneo ya kijeshi
Rais William Ruto apendekeza adhabu ya kifo kwa wauzaji wa dawa za kulevya
Nigeria yaagiza msako mkali baada ya watu wenye silaha kufanya mauaji katika jimbo la Niger
Tanzania yaaga mashindano ya AFCON 2025
Radi yaua watu wawili na kuwajeruhi wengine 150 nchini Afrika Kusini
AU inaeleza 'wasiwasi mkubwa', Afrika Kusini inaomba mkutano wa dharura wa UN juu ya Venezuela
Madaktari wa Sudan wanaonya kuhusu tishio la janga la kibinadamu kusini mwa Kordofan
Kenya yaomboleza ndovu maarufu 'super tusker' Craig, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 54
Zambia kuwa mwenyeji wa mkutano wa mawaziri wa ulinzi kuhusu mzozo wa DR Congo
Mapigano mapya yamezuka kati ya vikosi vya DRC na waasi wa M23 karibu na mji muhimu wa Uvira