25 Septemba 2025
Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi, Haji Ambar Khamis, amekiri kuwa yapo mazuri mengi yaliyofanywa na serikali ya nchi hiyo, ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, lakini ameongeza kusema kuwa, baadhi ya watendaji sio wazuri hivyo wanampotosha Rais.