16 Septemba 2025
Katika historia ya siasa na kinyang’anyiro cha uchaguzi nchini Tanzania, unapotaja vyama vya upinzani huwezi kukamilisha orodha bila kutaja Chama cha Wananchi – Civic United Front (CUF).
Hapo kabla CUF imeshiriki katika Uchaguzi Mkuu mara 6, ni mara 5 tu ndio ilisimika mgombea wa Urais na kushindwa mara zote. Na huyu ndiye Gombo Samandito Gombo aliyeteuliwa kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka 2025.