29 Oktoba 2025
Raia wa Tanzania kutoka sehemu mbalimbali za nchi wameanza kupiga kura mapema hii. Zoezi hilo limeanza rasmi saa moja asubuhi na linatarajiwa kukamilika saa kumi alasiri.
TRT Afrika, imekita kambi jijini Dodoma na kushuhudia zoezi hilo likiendelea kwa utulivu, ingawa mwitikio unaonekana kuwa mdogo ikilinganishwa na uchaguzi uliopita.
