4 Desemba 2025
Ingawa uvunaji wa madini hayo haujaanza, lakini fursa za ajira na ukuaji wa miundombinu muhimu kama vile vituo vya afya umeanza kuonekana kwa wananchi ambao awali hawakupata huduma hizo.
Iwapo uchimbaji huo utafanyika, basi Tanzania itakuwa miongoni mwa mataifa yanayochimba Helium. Hata hivyo, wadau mbalimbali, wanaitaka Serikali ya Tanzania kuweka mkakati madhubuti wa kuhakikisha mradi huo, unakuwa na tija kwa wananchi.

