| Swahili
Uganda: Biashara ya usafiri si ya watu binafsi
04:17
Afrika
Uganda: Biashara ya usafiri si ya watu binafsi
Uganda imepitisha sera mpya ya serikali ya kupiga marufuku wawekezaji binafsi katika usafiri wa umma. Sera hiyo mpya inafuatia kuongezeka kwa ajali za barabarani ambazo zinahusishwa na magari yaliyo katika hali hatari ya kiufundi na utovu wa nidhamu
4 Desemba 2025

Kwa zaidi ya miaka kumi na mitano kubeba abiria jijini Kampala, nchini Uganda kimekuwa ni chanzo kikuu cha mapato kwa Ali Kabuye. 

Kupitia mkopo aliweza kununua gari yenye uwezo wa kubeba abiria kumi na wanne. 

Lakini sasa wasiwasi wake ni athari ya agizo jipya la serikali la kuzuia umiliki binafsi wa magari hayo.

"Tuna mifumo yetu ya kuweka akiba na tayari tunao wadhamini wa mikopo katika biashara hii,” Kabuye ameambia TRT Afrika.

“ Pendekezo la kujiunga na miradi mipya na kununua magari mapya ni njama ya kutuondoa kwenye biashara, kwa sababu magari mapya yaliyonunuliwa kwa mkopo yatatufanya kuwa wafanyakazi wao, ukipata dharura huwezi kutumia fedha zao, " anaelezea.

Mei 12, 2024, serikali ya Uganda iltangaza kuwa biashara ya kusafirisha abiria jijini kamapala na maneneo mengi ya nchi hii iwe chini ya wanaomiliki magari kwa vikundi pekee.

Tazama Video zaidi
Tanzania yaingia katika orodha ya nchi zinazozalisha gesi ya Helium
Afrika ndilo bara la pili katika uzalishaji wa asali duniani | Utajiri wa Afrika
Charles Kibe Mwangi na simulizi ya njiti ya ufagio
Je, unaijua nchi ya Iran?
Je, Ufaransa Ilifanya nini Cameroon? Ukweli wafichuka
Raila Odinga asimulia alivyotumia pasipoti ya Tanganyika kusafiria
Eunice: 'Mimi naweza chochote' | Story Yangu
Bwana Chui Bin Kositi: Shujaa wa Uadilifu kutoka Congo
Wanafunzi wasichana wapata mafunzo ya teknolojia nchini Kenya
Kenya na mabaki na makovu kutoka kwa mateso ya Malaika wa Kuzimu wa BATUK