Kwa zaidi ya miaka kumi na mitano kubeba abiria jijini Kampala, nchini Uganda kimekuwa ni chanzo kikuu cha mapato kwa Ali Kabuye.
Kupitia mkopo aliweza kununua gari yenye uwezo wa kubeba abiria kumi na wanne.
Lakini sasa wasiwasi wake ni athari ya agizo jipya la serikali la kuzuia umiliki binafsi wa magari hayo.
"Tuna mifumo yetu ya kuweka akiba na tayari tunao wadhamini wa mikopo katika biashara hii,” Kabuye ameambia TRT Afrika.
“ Pendekezo la kujiunga na miradi mipya na kununua magari mapya ni njama ya kutuondoa kwenye biashara, kwa sababu magari mapya yaliyonunuliwa kwa mkopo yatatufanya kuwa wafanyakazi wao, ukipata dharura huwezi kutumia fedha zao, " anaelezea.
Mei 12, 2024, serikali ya Uganda iltangaza kuwa biashara ya kusafirisha abiria jijini kamapala na maneneo mengi ya nchi hii iwe chini ya wanaomiliki magari kwa vikundi pekee.

