11 Septemba 2025
Mgombea Ubunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amemnadi Kiza Mayeye, mgombea wa Kigoma Kaskazini kupitia chama hicho, akisisitiza umuhimu wa kushinda majimbo yote ya Mkoa wa Kigoma kwa ajili ya kuleta mabadiliko.
Akizungumza Septemba 08, 2025, katika uzinduzi wa kampeni Kigoma Kaskazini, Zitto alisema Kigoma bado iko nyuma kimaendeleo, hivyo ushindi wa ACT katika mkoa mzima ni muhimu.