AFRIKA
1 dk kusoma
Ajali ya treni mashariki mwa Ethiopia yaua watu 14, wengine 29 wajeruhiwa
Watu wasiopungua 14 wamefariki dunia na wengine 29 kujeruhiwa baada ya treni ya abiria kupata ajali mashariki mwa Ethiopia, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa Jumanne na vyombo vya habari vya serikali.
Ajali ya treni mashariki mwa Ethiopia yaua watu 14, wengine 29 wajeruhiwa
Ajali ya treni nchini Ethiopia imeua watu 14 mnamo Oktoba 21, 2025. / / Reuters
tokea masaa 16

Ajali hiyo ilitokea majira ya saa nane usiku wakati treni hiyo ilikuwa safarini katika safari ya takriban kilomita 200 kutoka mji wa Dewele, ulioko karibu na mpaka wa Djibouti, kuelekea mji wa Dire Dawa. Maafisa wa eneo hilo walieleza kuwa ajali hiyo ilisababisha maafa makubwa kwa abiria waliokuwa wakisafiri na treni hiyo.

"Ajali iliyotokea katika reli ya Dire Dawa-Dewele imewaua watu 14 na kujeruhi wengine 29, baadhi yao wakiwa na majeraha makubwa," ilieleza taarifa ya Dire TV iliyochapishwa kwenye ukurasa wao wa Facebook, bila kutoa maelezo ya kina kuhusu chanzo cha ajali hiyo.

Picha zilizosambazwa na chombo hicho cha habari zilionyesha mabehewa ya treni yakiwa yamepinduka, mengine yakiwa yamesvunjika, jambo linaloashiria ukubwa wa tukio hilo.

Ajali za treni si za kawaida nchini Ethiopia

Ajali za treni si jambo la kawaida nchini Ethiopia, taifa lenye idadi ya watu takriban milioni 130, na ambalo linashikilia nafasi ya pili kwa idadi ya watu barani Afrika.

Ajali kubwa ya mwisho ya treni nchini humo iliripotiwa mwaka 1985, ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha na wengine 500 kujeruhiwa baada ya treni iliyokuwa ikitokea Djibouti kuelekea Addis Ababa kuanguka kwenye korongo.

CHANZO:AFP