Brian Okoth
Kauli hiyo ya Waziri wa Kenya kwa aina ya uongozi wa Rwanda na ukubwa wa nchi hiyo, imesababisha ukosoaji mkubwa ndani na nje ya nchi.
Disemba 18, Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen aliita Rwanda kama taifa "linalotawaliwa na mtu mmoja" katika mahojiano na kituo binafsi cha runinga, Citizen.
Alisema kwamba, nchini Rwanda, kauli ya rais ni sheria.
Murkomen aliulizwa kwa nini Kenya haiwezi kuboresha usafiri wake wa umma na kufanya kazi katika misingi bora kama ilivyo nchini Rwanda.
Serikali ya Kenya, kwa mara kadhaa, imekuwa ikionyesha wasiwasi wake kutokana na ukosefu wa usalama katika sekta ya usafiri wa umma.
Rwanda ni taifa la 'kidugu'
Katika kujibu, Murkomen alisema: "Hapa (nchini Kenya), watu wanasababisha vurugu, wanaenda kotini, … Kwa hiyo, kila uamuzi unaochukua nchini humu, lazima kwanza uwasilishe pendekezo, halafu bungeni, halafu ushirikishwaji wa wananchi, na baada ya kupitia mchakato wote huo, utahitajika upitie mahakamani…"
Waziri alikuwa na maana kwamba, kuendesha sekta ya usafiri wa umma Rwanda ni rahisi kwa sababu "nchi hiyo ni ndogo" kwa idadi ya watu.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Korir Sing'oei katika hali ya kutuliza mambo alikimbilia katika mtandao wa kjamii wa X na kuiita Rwanda taifa la "Kidugu," na kwamba Rais wa Rwanda Paul Kagame alikuwa ni "kiongozi wa kupigiwa mfano ambae uongozi wake unavutia ndani na nje."
Kiongozi wa upinzani wa Kenya Raila Odinga amemkosoa Murkomen, amesema katika taarifa yake ya Disemba 19 kwamba kauli hiyo ya Waziri inaweza kuharibu uhusiano wa Kenya na Rwanda.
'Mtizano, sio ukubwa unaojenga nchi'
"Lugha iliyotumiwa dhidi ya nchi muhimu na watu wake wa Rwanda ni ya kusikitisha… sio ukubwa unaotengeza nchi, lakini ni maono na uogozi," Odinga amesema.
Je, Rwanda ni ndogo kuliko kaunti ya Kajiado kama inavyodaiwa na Waziri? Jibu ni hapana.
Kaunti ya Kajiado, inayopakana na mji mkuu wa Kenya Nairobi kwa upande wa kusini, ni mita za mraba 21,293 kwa ukubwa, na ina watu zaidi kidogo ya 1.1.
Rwanda, iliyo kusini magharibi mwa Kenya, ina kilomita za mraba 26,338, na idadi ya watu zaidi kidogo ya milioini 13
Utawala wa mtu mmoja?
Ni sawa sawa na ukubwa wa Burundi, Albania na Haiti, na kwa makadirio ni kubwa mara 36 ya Singapore.
Je, Rwanda ina mfumo wa kutawaliwa na mtu mmoja. Mfumo huo wa serikali wa mtu mmoja huwa na mamlaka ya kupindukia juu ya wengine.
Rwanda inafanya uchaguzi wake kila mara kukidhi mahitaji ya nchi yenye demokrasia, na vile vile ina bunge la wananchi ambalo "linaangalia utendaji wa serikali kwa niaba ya wananchi wa Rwanda." Hata hivyo, wakosoaji wanadai kwamba, mamlaka ipo mikononi mwa wachache.
Kwa upande wa biashara, Rwanda inajihusisha vipi na Kenya? Nchi mbili hizo ni washirika wakubwa wa biashara, huku rekodi zikionyesha kwamba Rwanda ni muuzaji mkubwa wa bidhaa nje kwa Kenya barani Afrika, ikifuatiwa na Tanzania na Uganda.
Soko muhimu la Kenya
Mwaka 2022, Kenya imepeleka bidhaa zenye thamani ya dola 295 milioni Rwanda, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Wanyama, mafuta ya mboga, chuma, plastiki, karatasi ni miongoni mwa bidhaa zinazoongoza kupelekwa Rwanda.
Rwanda, kwa upande wake, imepeleka bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 12 ikiwa ni pamoja na unga, maziwa, viungo vya kupikia, kahawa na chai.