| Swahili
UTURUKI
2 DK KUSOMA
Erdogan afanya mazungumzo ya simu, ajadili masuala ya kanda na dunia
Rais wa Uturuki alizungumza na wenzake wa Uzbek na Iraqi na pia kufanya mazungumzo ya simu ya Waziri Mkuu wa Pakistan kuhusu ushirikiano, juhudi za kupambana na ugaidi na masuala ya kikanda na kidunia.
Erdogan afanya mazungumzo ya simu, ajadili masuala ya kanda na dunia
Pia, Erdogan alituma salamu zake za rambirambi kufuatia vifo vilivyotokana na ugaidi nchini Pakistan , and “kuonesha imani yake kuwa Pakistan itashinda kipindi hicho kigumu kutokana na uzoefu wake,” ilisema kurugenzi hiyo./ Picha: AA   / Others
10 Aprili 2024

Rais wa Uturuki amefanya mazungumzo ya simu na viongozi wenzake wa Uzbekistan na Iraq na waziri mkuu wa Pakistan kujadili uhusiano wa nchi mbili, juhudi za kukabiliana na ugaidi na masuala ya kikanda.

Simu kati ya Recep Tayyip Erdogan na Abdul Latif Rashid wa Iraq na Shavkat Mirziyoyev wa Uzbekistan ziliangazia uhusiano wa nchi mbili pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa, kulingana na taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki kwenye ukurasa wa X, siku ya Jumanne.

Wakati huo huo, simu kati ya Erdogan na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif iliangazia uhusiano wa nchi mbili na maswala ya kimataifa.

Pia, Erdogan alituma salamu zake za rambirambi kufuatia vifo vilivyotokana na ugaidi nchini Pakistan , and “kuonesha imani yake kuwa Pakistan itashinda kipindi hicho kigumu kutokana na uzoefu wake,” ilisema kurugenzi hiyo

Rais huyo wa Uturuki pia alipeana salamu za sikukuu ya Eid pamoja na wenzake wa Iraqi na Uzbek na Waziri Mkuu wa Pakistan.

Sikukuu ya Eid al Fitr huashiria mwisho wa mwezi wa mfungo wa Waislamu wa Ramadhan.

CHANZO:TRT Afrika