| Swahili
ULIMWENGU
2 DK KUSOMA
Vyuo vikuu vya Uturuki vyaunga mkono maandamano ya Wapalestina katika vyuo vikuu vya Marekani
Taarifa ya pamoja ya vyuo vikuu 16 inasema kwamba mwitikio usio na uwiano kwa maandamano ya amani ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Marekani ni "pigo kwa haki za kimsingi za binadamu na uhuru wa kitaaluma.
Vyuo vikuu vya Uturuki vyaunga mkono maandamano ya Wapalestina katika vyuo vikuu vya Marekani
Maandamano ya wanafunzi kuhusu vita vya Israel dhidi ya Gaza yameibuka katika idadi inayoongezeka ya vyuo vikuu kufuatia kukamatwa kwa zaidi ya waandamanaji 100 katika Chuo Kikuu cha Columbia wiki iliyopita. / Picha: AP / Others
25 Aprili 2024

Vyuo vikuu nchini Uturuki vimejitokeza kupinga matumizi yasiyolingana na nguvu inayotumika na polisi dhidi ya wanafunzi wanaopinga kinachoendelea Gaza.

Maandamano hayo yanaendelea Marekani kwa sasa.

"Kwa zaidi ya miezi 6, vurugu zimekuwa zikitumiwa dhidi ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wamekuwa wakipinga kwa amani matukio ya kikatili yanayolenga kuharibu watu wasio na hatia wanaoishi Gaza," taarifa za pamoja za vyuo vikuu 26 zilisema.

Walibainisha kuwa baadhi ya wanafunzi wamekamatwa, na vyuo vikuu vimechagua kufanya masomo kwa njia ya mtandao ili kuzuia maandamano.

Kwanzia Chuo Kikuu cha Columbia hadi Yale, Chuo Kikuu cha New York hadi Harvard, waandamanaji wamekuwa wakidai kwamba vyuo vyao viunge mkono wito wa kusitisha mapigano huko Gaza na kuvunja uhusiano na makampuni yanayohusiana au kushirikiana na Israel.

Vita vya Israel dhidi ya Gaza viko katika siku ya 202, vimeua takribani Wapalestina 34,262 - asilimia 70 yao wakiwa ni watoto na wanawake - na kuwajeruhi zaidi ya watu 77,229.

CHANZO:TRT World