Kanda ya Afrika Mashariki inajivunia kuwa na Ziwa kubwa zaidi barani Afrika na Ziwa kubwa zaidi la kitropiki duniani. Kwa ukubwa, Ziwa Victoria ni la 9 duniani.
Miji mikuu inayounganisha Ziwa Victoria ni Entebbe nchini Uganda, Mwanza nchini Tanzania, Kisumu nchini Kenya na mji wa Musoma ulioko kaskazini mwa Tanzania karibu na mpaka wa Kenya kwenye mwambao wa Ziwa Victoria.
Ziwa Victoria pia linajulikana kwa majina ya Ziwa Nyanza, Nam Lolwe (Luo) na Nnalubaale (Luganda).
Ina kina kifupi na kina cha juu cha kati ya mita 80 hadi 84 na kina cha wastani cha mita 40.
Kiasi chake cha maji ni kidogo ikilinganishwa na maziwa mengine makubwa barani Afrika. Ikiwa na kilomita za ujazo 2424 za maji.
Kiasi cha asilimia 85 ya maji yanayojaza Ziwa Victoria hutokana na mvua na karibu asimilia 15 ya maji hupotea kwa uvukizi.
Lina fukwe yenye urefu wa kilomita 3440 na takriban watu milioni 30 wanaoishi katika Bonde la Ziwa.
Ziwa Victoria, lina idadi kubwa ya viboko na mamba. Wote ni hatari na wanaripotiwa kuwa chanzo cha vifo vya mamia ya watu.
Visiwa vya Ziwa Victoria ni vivutio vikuu na wasafiri wengi hutembelea kanda ya ziwa kwa shughuli mbalimbali, ikiwemo uvuvi.
Kuna Visiwa vya Ssese. Visiwa hivi vya ajabu vinaundwa na visiwa 84 na viko katika sehemu ya kaskazini-magharibi mwa Ziwa Victoria ambayo iko ndani ya Uganda.
Mto Kagera ndio mto mkubwa unaopita katika Ziwa Victoria. Mito miwili inatoka kwenye ziwa kubwa: White Nile au Victoria Nile na Katonga River.
Kutoka maporomoko ya maji ya Ripon karibu na Jinja nchini Uganda, maji ya Ziwa yanatiririka kuelekea kaskazini kwa kilomita 500. Maporomoko ya Murchison, yanatiririka katika Ziwa Albert na kuingia Albert Nile.
Hii ni sehemu ya mwisho ya mto nchini Uganda kabla ya kuingia Sudan.
Mto pekee unaotoka katika Ziwa Victoria ni Mto Nile. Ziwa Victoria ndiyo chanzo kikuu cha maji zaidi ya Mto Nile.
Kwa jumla, kuna visiwa vidogo vidogo zaidi ya 3,000 ambavyo havikutajwa katika Ziwa Victoria.
Ziwa pekee la maji safi ambalo ni kubwa kuliko Ziwa Victoria ni Ziwa Superior huko Amerika Kaskazini.
Uganda inaendesha mabwawa mawili makubwa ya kuzalisha umeme kwenye Ziwa Victoria.
Ziwa Victoria linasaidia sekta kubwa ya uvuvi barani Afrika. Samaki wanaovuliwa katika Ziwa Victoria ni pamoja na spishi za kiasili kama vile tilapia na cichlids za haplochromine pamoja na spishi za kigeni kama vile sangara wa Nile, samaki aina ya silver butter catfish, elephant fish na marbled lungfish.
Uvuvi wa Nile Perch ulianzishwa miaka ya 1950 ili kukuza sekta ya uvuvi na hii imesababisha matatizo makubwa kwani samaki hao ni vamizi sana.
Katika kilele chake mwanzoni mwa miaka ya 1990, tani 500,000 za sangara wa Nile zilivunwa kila mwaka katika Ziwa Victoria lakini hii imepungua sana katika miaka ya hivi karibuni kutokana na uvuvi wa kupita kiasi.
Hata hivyo, kuna wasiwasi sasa kwani Ziwa kubwa linakabiliwa na masuala kadhaa muhimu ya kimazingira, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa magugu maji, uvuvi wa kupita kiasi, ukataji miti wa misitu ya visiwa na uchafuzi wa maji.













