| swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
Sudan Kusini yakumbwa na ugonjwa wa Mpox
Hii ni kufuatia taarifa za mtu mmoja kukutwa na ugonjwa huo, baada ya kuwa ametokea nchini Uganda, ambapo maradhi hayo yamekuwepo toka mwaka 2024
Sudan Kusini yakumbwa na ugonjwa wa Mpox
Kaimu Waziri wa Afya wa nchi hiyo James Hoth Mai, alisema siku ya Ijumaa kuwa, mtu huyo alikutwa na dalili za homa, vipele na mwili kuwashwa./Picha: Reuters
7 Februari 2025

Sudan Kusini imethibitisha mlipuko wa ugonjwa wa Mpox, baada ya mtu mmoja kugundulika na virusi hivyo.

Kaimu Waziri wa Afya wa nchi hiyo James Hoth Mai, alisema siku ya Ijumaa kuwa, mtu huyo alikutwa na dalili za homa, vipele na mwili kuwashwa.

“Wizara ingependa kuutarifu umma juu ya mlipuko wa mpox,” alisema Waziri huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Juba.

Kulingana na Mai, maabara kuu ya nchi hiyo ilimfanyia vipimo raia mmoja wa Uganda ambaye pai ni mkazi wa eneo la kambi ya Kupuri, iliyoko Luri Payam, jijini Juba na kumkuta na dalili hizo.

Waziri huyo amesema kuwa, mgonjwa huyo alisafiri kwenda Uganda, hivi karibuni.

Aidha, ameongeza kwa kusema kuwa Wizara ya Afya ya nchi hiyo imejipanga kuratibu namna ya kukabiliana na ugonjwa huo.

“Mgonjwa huyo amewekwa sehemu maalumu katika hospitali ya Gudele. Timu ya wataalamu iko kazini kwa ajili ya uchunguzi na ufuatiliaji zaidi kuhusiana na mlipuko wa ugonjwa huo,” aliongeza.

Mai amewataka wahudumu wa afya kujipanga kukabiliana na maradhi hayo na pia kutoa taarifa mapema pindi watakapohisi uwepo wa maambukizi zaidi.

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
UN yaagiza uchunguzi wa dharura ufanyike kuhusu ukiukaji wa sheria katika Al Fasher ya Sudan
Rais wa Tanzania atangaza uchunguzi kuhusu mauaji ya waandamanaji katika uchaguzi
Wakimbizi 57,000 wamewasili kaskazini mwa Sudan baada ya mashambulizi ya RSF huko Darfur, Kordofan
Afrika Kusini yaruhusu kuingia kwa wakimbizi zaidi ya 150 kutoka Gaza, Palestina
Afrika yakumbwa na mlipuko wa kipindupindu mbaya zaidi katika miaka 25
Mataifa ya G7 walaani mashambulizi ya RSF dhidi ya raia Sudan, watoa wito wa kusitishwa mapigano
Wakenya zaidi ya 200 wajiunga na jeshi la Urusi
AU yakanusha tuhuma za Trump kuhusu mauaji ya halaiki Nigeria
Mwigulu Nchemba ateuliwa Waziri Mkuu Tanzania
Jaji Mkenya achaguliwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amfuta kazi makamu wake
Duma wa Botswana aipa India zawadi ya duma 8
Kesi ya Roger Lumbala wa DRC yaanza kusikilizwa
Kesi za ubakaji, watoto kupotea zaripotiwa Darfur, Sudan – Umoja wa Mataifa
Ugonjwa wa Kichaa cha mbwa barani Afrika: Janga linaloendelea kuathiri maisha japo linaepukika
Libya yatakiwa kufunga vituo vya kuwazuilia wahamiaji katika mkutano wa Umoja wa Mataifa
Rais Museveni aonya kuzuka kwa vita endapo nchi za Afrika zitashindwa kufikia Bahari ya Hindi
UN: Milioni 11 wanawake na wasichana wanabeba uzito mkubwa wakati njaa ya Sudan inaendelea kupamba moto
Ethiopia yachagguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa, COP32
Ghana yafichua sababu ya ajali ya helikopta iliyoua watu wanane, wakiwemo mawaziri, mwezi Agosti