Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, siku ya Ijumaa aliadhimisha kumbukumbu ya miaka 81 ya kuwa uhamishoni kwa Waturuki Wahiska kutoka katika eneo la (Akhaltsikhe/Meskheti) nchini Georgia, na vifo vyao mwaka 1944.
“Mioyoni mwetu bado tuna uchungu wa watu wapatao laki moja walioondolewa kutoka ardhi yao ya asili Novemba 14, 1944,” alisema Erdogan kwenye mtandao wa kijamii wa Uturuki wa NSosyal.
Aliwaombea watu hao huruma ya Mungu, akiongeza kuwa bado ana maumivu ya waliyopitia Waturuki Wahiska kwenye kumbukumbu ya miaka 81.
Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilisema kuwa, mnamo Novemba 14, watu wapatao 100,000 waliondolewa kutoka kwenye maeneo yao katika eneo la Ahiska ndani ya jamhuri iliyokuwa ya Kisovietu ya Georgia, yenye kupakana na Uturuki na kupelekwa kwenye maeneo ya ndani zaidi.
Maelfu ya watu walipoteza maisha kwa njaa, baridi na magonjwa kwenye safari hiyo ya mateso, taarifa hiyo iliongeza.
“Kwenye kumbukumbu hii ya miaka 81, tunakumbuka kwa masikitiko makubwa janga hili kubwa na kwa heshima zote tunawakumbuka ndugu zetu waliopteza maisha wakiwa uhamishoni,” ilisema taarifa hiyo.
Iliongeza kuwa, licha ya mates ohayo, watu hao waliweza kuhifadhi utambulisho wao, lugha, imani na kufanikiwa kurithisha kwa vizazi vingine.
Kwa upande mwingine, Uturuki imesema kuwa inatumai kuwa mchakato wa wa kuwawezesha Waturuki Meskhetian kurejea kwenye makazi yao ya asili, utakuwa wa mafanikio.
Uhamisho wa 1944
Mnamo Novemba 14, 1944, mamlaka za Kisovieti, ziliwatuhumu wakazi wa Akhaltsikhe, ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Meskheti, kuhusika na tishio la amani.
Ndani ya saa chache, zaidi ya watu 90,000, wakiwemo wanawake, watoto na wazee waliondolewa kwenye nyumba zao na kupakiwa kwenye magari ya mizigo.
Watu hao walisafirishwa kwa mwezi mmoja kuelekea maeneo ya kati ya Asia, huku 17, 000 kati ya hao, wakipoteza maisha kutokana na njaa, baridi na magonjwa.



























