Kocha wa timu ya taifa ya Wales, Craig Bellamy ameonya kuwa mshambuliaji mkongwe wa Bosnia na Herzegovina, bado anabaki kuwa tishio wakati timmu yake ikisaka nafasi ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia.
Dzeko, ambaye ameshinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya Uingereza akiwa na Manchester City, atatimiza miaka 40, Jumanne, siku ambayo Bellamy anatarajiwa kutangaza kikosi chake kwa ajili ya mechi za kufuzu michuano hiyo mikubwa ulimwenguni.
Wales itakuwa mwenyeji wa Bosnia katika mchezo utakaofanyika Machi 26, jijini Cardiff.
Kwa sasa, Dzeko anaichezea klabu ya Schalke inayoshiriki Ligi Kuu ya Bundesliga ya nchini Ujerumani.
Kabla ya hapo, Dzeko ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Bosnia, aliwahi kuzichezea klabu za Inter Milan na Roma za nchini Italia.
"Japo hana kasi, lakini ana akili nyingi pindi awapo uwanjani," alisema Bellamy, nyota wa zamani wa Manchester City.
"Bado anacheza katika kiwango kizuri na ni mchezaji hatari.
"Lengo letu litakuwa ni kuwaweka Bosnia mbali na eneo letu ili kuepusha hatari yoyote ile. Tukifanikiwa hilo, basi itakuwa na faida kwetu."



















