| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Polisi wa Kimataifa wawakamata watu 651 Afrika kwa utapeli wa kutumia simu wa dola milioni $45
Operesheni hiyo imefanyika katika nchi za Angola, Benin, Cameroon, Chad, Gabon, Gambia, Ghana, Ivory Coast, Kenya, Namibia, Nigeria, Rwanda, Senegal, Uganda, Zambia na Zimbabwe.
Polisi wa Kimataifa wawakamata watu 651 Afrika kwa utapeli wa kutumia simu wa dola milioni $45
Mamlaka zilipata vifaa vya kielektroniki 2,341 na kuzima vyanzo tata 1,442 vya mitandao, pamoja na miundombinu mengine. Picha / Interpol / Wengine
tokea masaa 11

Polisi katika nchi 16 za Afrika wamekamata watu 651 katika wiki za hivi karibuni, na kuvunja mtandao wa uhalifu wa mtandaoni ambao umekuwa ukiiba mamilioni ya dola kutoka kwa watu, Interpol imesema.

Zoezi hilo la wiki nane limesambaratisha mtandao ambao umeiba zaidi ya dola milioni 45 kutoka kwa maelfu ya watu - wengi wao kutoka Afrika, kwa mujibu wa Polisi wa Kimataifa wa Interpol.

Wizi wa mitandaoni unatokana na utapeli wa uwekezaji, wizi wa kwenye simu, na maombi ya utapeli ya mikopo, imesema.

Wachunguzi pia wamekamata vifaa 2,341 na kufunga vyengine 1,442.  Msako huo umefanyika kati ya mwezi Disemba na Januari.

‘Ahadi za uongo’

"Uhalifu huu wa mitandaoni unasababisha madhara makubwa ya kifedha kwa watu, biashara na jamii nzima kwa ujumla kwa ahadi za uongo," amesema Neal Jetton, mkuu wa kurugenzi ya uhalifu wa mitandaoni wa Interpol.

"Nawahimiza waathirika wote wa uhalifu wa mitandaoni kutafuta msaada wa kisheria," ameongeza kusema.

Nchi zilizofanyiwa msako ni Angola, Benin, Cameroon, Chad, Gabon, Gambia, Ghana, Ivory Coast, Kenya, Namibia, Nigeria, Rwanda, Senegal, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

CHANZO:TRT Afrika Swahili