Katika Fainali ya AFCON 2025 Sadio Mane alionesha umuhimu wa kuwa kiongozi akienda kinyume na maagizo ya kocha wake Pape Bouna Thiaw.
Kwa kiasi fulani ubingwa wa pili wa Senegal AFCON unanasibishwa na Sadio Mane.Haikuwa ajabu pale winga huyo mwenye umri wa miaka 33 alipochaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano ya AFCON ya mwaka huu.
Tangu kuanza kwa michuano hii Sadio Mane ameonekana kuwa makini na namna anavyosherehekea na namna anavyoamiliana na wachezaji wenzake ndani na nje ya uwanja.
Pale unapohitajika utaitwa na uongozi alivyoonesha kuwarejesha wachezaji wenzake uwanjani ilikuwa ni jambo linasemekana kuwa la hekima ya hali ya juu, kama vile akiwaambia ‘msisuse, njooni tupambane’ na naam mwisho wa siku ubingwa ukawa wa Simba wa Teranga.
Simba wa Atlas alionekana kunywesha chai na kutulizwa hasa pale Brahim Diaz alipokosa mkwaju kwa penati kwa timu hiyo ya wenyeji.
Mane mwenyewe alimakinika na kuwataka wachezaji kupambania kombe. Mzaliwa wa kijiji cha Bambali, kwa mara nyingine tena ameibeba timu ya Senegal, na kudhihirisha kuwa taifa hilo la Afrika Magharibi ndiyo kisiki cha mataifa ya Afrika Kaskazini, si Misri wala Morocco.
Kocha Pape Thiaw anasema licha ya Mane kutangaza kuwa huenda ikawa AFCON yake ya mwisho, anasema hilo si kwa Sadio kuamua kutokana na mchango wake kuhitajika zaidi.
Sadio Mane, winga machachari, busara ya hali ya juu na mbeba matumaini ya Simba wa Teranga.
Je, alionesha kweli jogoo wa shamba anaweza kuwika mjini?













